Nusra Maguluko Mwanamke Pekee Dereva wa Mabasi ya Mikoani

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bila, Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mkurugenzi wa DHL na Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar, Rashid Seif Suleiman, wakiwa katika picha ya pamoja na Nusra Maguluko, wakati wa hafla ya uzinduzi wa jingo la DHL, hivi karibuni.

Dereva Mwanamke wa Basi la Shabiby, Nusra Maguluko akiwa kazini

Dereva Mwanamke wa Basi la Shabiby, Nusra Maguluko akiwa kazini

NUSRA Maguluko (28) ni msichana jasiri na anayependa kujaribu na kupata mafanikio ya majaribio yake bila woga wala kujali ni aina gani ya kazi anayotakiwa kufanya yeye kama mwanamke na ipi asiyostahili kufanya yeye kama mwanamke.

Ni ujasiri wake hasa ndiyo ulimuwezesha kumfikisha hatua aliyonayo kwa sasa, ambaye ni miongoni mwa wanawake wachache na hasa kwa Tanzania waliopata kuifikia na kujiamini hadi kuwa na ujasiri wa kubeba roho za watu zisizopungua 40 kila safari moja ya kwenda Dodoma ama kotoka Dodoma kuja Dar.

Nusra ni mzaliwa wa Mkoa wa Manyara katika wilaya ya Kiketo, na ni mtoto wa nne kuzaliwa kati ya 12 wa familia ya baba yake mzazi mzee, Maguluko na Elimu yake ni Kidato cha pili tu.
Alimaliza elimu ya Msingi mwaka 1997, katika Shule ya Msingi Matui iliyoko Wilayani Kiteto, baada ya kuhitimu elimu ya msingi alijiunga na elimu ya Sekondari ambayo kwa bahati mbaya hakuweza kumaliza na kuishia Kidato cha pili baada ya kusumbuliwa na maumivu ya kichwa mara kwa mara.

Nusra, alishauriwa na madaktari kupumzika kwa muda wa miaka mitatu bila kusoma ama kuwa akiangalia karatasi nyeupe mara kwa mara, jambo ambalo lilimfanya kuamua kumsumbua Baba yake mkubwa, Hamis Mang’endi aliyekuwa ni fundi wa magari ili amfundishe ufundi na udereva wa gari.

Baada ya kumsumbua sana baba yake mkubwa, kwa kuwa akiripoti katika gereji yake kila asubuhi na kushinda hapo huku akimfuatilia kila analofanya katika magari, Mzee Hamis, baada ya kuona kuwa Nusra alikuwa na moyo wa kweli wa kujifunza ufundi, aliamua kuanza kumfundisha ufundi hatua kwa hatua.

Chanzo: www.sufianimafoto.blogspot.com