Ikulu Yawazawadia Wafanyakazi, Wanamichezo bora 2012

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akinyanyua juu mojawapo ya makombe matano ambayo Ikulu Sports Club ilinyakua kwenye michezo ya SHIMIWI ya mwaka huu mjini Dodoma katika hafla ya kukabidhi makombe na kuwazawadia wafanyakazi bora iliyofanyika Desemba 17, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam. Kwenye michezo hiyo iliyofanyika kuanzia Septemba 22 hadi Oktoba 10 mwaka huu, ilishirikisha jumla ya wanamichezo 3500 kutoka wizara 56, mikoa 18 na idara za serikali 14 ambapo wanamichezo 91 wa Ikulu walioshiriki walifanikiwa kuibuka washindi wa kwanza katika michezo ya Baiskeli, Netbal, Kuvuta kamba wanawake na wanaume na kushik nafasi ya pili ya riadha kwa wanawake na wanaume.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akimpa zawadi Bw. Miraji Ahmed Saleh kwa kuibua mfanyakazi bora na pia mfanyakazi hodari wa Ofisi ya Rais Ikulu. Bw Saleh ni Msaidizi wa Ofisi Mwandamizi katika Idara ya Huduma za Ikulu na Zahanati katika hafla ya kuwazawadia iliyofanyika Desemba 17, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (wa nane toka kulia ) pamoja na Naibu Katibu Mkuu Ikulu Mama Suzana Mlawi (kulia kwake) na Mkurugenzi wa Huduma za Ikulu Bw Julius Mogore (wa pili kushoto ) pamoja na mwenyekiti wa TUGHE tawi la Ikulu Bw. Paulo Mgeni (kulia) wakiwa na Mwadawa Twalibu, Sophie Komba na Pascalia Kibayasa ambao wachezaji wa timu ya netball ya Ikulu Sports Club ambao pia ni wachezaji wa timu ya taifa ya mchezo huo (Taifa Queens) kwenye hafla ya kuwazawadia iliyofanyika leo Desemba 17, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (wa nane toka kulia ) pamoja na Naibu Katibu Mkuu Ikulu Mama Suzana Mlawi (kulia kwake) na Mkurugenzi wa Huduma za Ikulu Bw Julius Mogore (kushoto kwake) wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi bora wa Ofisi ya Rais, Ikulu katika hafla ya kukabidhi makombe na kuwazawadia wafanyakazi bora iliyofanyika leo Desemba 17, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam