RAIS wa Madagascar, Andry Rajoelina ambaye amewasili mjini Dar es Salaam mchana Desemba 14 kwa ziara ya kikazi ya siku mbili nchini akiwa na Mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, Ikulu, tayari kuanza mazungumzo rasmi.
Rais Kikwete ni Mwenyekiti wa Tume ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya
Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ambapo amepewa jukumu na viongozi wenzake ndani ya Jumuiya hiyo kukutana na viongozi wa
Madagascar kuwaelezea maamuzi ya mkutano wa viongozi hao wa SADC
uliofanyika mwishoni mwa wiki mjini Dar Es Salaam.Kwenye mkutano na
waandishi wa habari uliofanyika Ikulu, Dar Es Salaam, mwanzoni mwa wiki hii, Ravalomanana alithibitisha kuwa amekubaliana na maamuzi ya viongozi wa SADC.
Miongoni mwa mambo mengine, viongozi hao wa SADC wanataka viongozi hao wawili wa Madagascar washawishiwe na wakubali kutogombea katika
Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika nchini humo mwakani.