Mabondia Miyeyusho na Ramadhani Kuwania Ubingwa wa Mabara WBF

Promota wa mpambano wa Ubingwa wa WBF Mohamed Bawaziri Katikati akiwa na mkanda wa ubingwa watakaogombania mabondia Nassibu Ramadhani kushoto na Fransic Miyayusho wakati wa utambulisho wa mpambano huo utakaofanyika katika Ukumbi wa PTA Sabasaba Desemba 9, 2012. (Picha na Super D blog)

WAKATI mabondia Francis Miyeyusho na Nassib Ramadhani wakitarajiwa kupima uzito Desemba 8 kabla ya kuvaana kuwania ubingwa wa Mabara wa WBF, viongozi waalikwa watakaoshuhudia pambano hilo wamefahamika. Promota wa pambano hilo litakalofanyika jijini Dar siku ya Desemba 9, Mohammed Bawazir alisema, miongoni mwa viongozi hao waalikwa ni Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk. David Mathayo.

Mgeni rasmi ni Waziri wa Hbari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara. Bawazir alisema, wengine waliothibitisha kushuhudia pambano hilo la uzani wa Bantam ni pamoja na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova na Katibu wa Itikidi na Uenezi-CCM, Nape Nnauye.

“Hao ni baadhi ya viongozi wakuu tuliowatumia mwaliko na kutuhakikishia watahudhuria na tutamtangaza mgeni rasmi siku ya Desemba 6,” alisema.

Promota huyo alisema wangependa mgeni rasmi katika pambano hilo awe mmoja wa viongozi wa juu wa Taifa na ndiyo maana
Juu ya maandalizi ya pambano hilo linalosubiriwa kwa hamu kutokana na ubora na rekodi za mabondia hao wawili, Bawazir alisema yanaendelea vema japo wamekwama kupata wadhamini wa kuwapiga tafu. Bawazir alisema pamoja na hayo bado wanaendelea kuitoa wito kwa watu wenye mapenzi mema na mchezo wa ngumi kujitokeza kuwapa nguvu, huku akisema upimaji wa uzito na afya kwa mabondia utafanyika Desemba 8. katika uwanja wa Karume.

“Maandalizi yaendelea vema japo wadhamini wanasuasua kujitokeza na mabondia wote watapimwa kupimwa uzito na afya zao Desemba 8, siku moja kabla ya kupanda ulingoni,” alisema.

Pambano hilo litafanyika chini ya usimamizi wa Shirikisho la Ngumi za Kulipwa Tanzania, PST na litatanguliwa na michezo kadhaa ya utangulizi.