Ofisi ya Shule ya Msingi Chini ya Mti Huu…!

Mti huu kivuli chake ni ofisi ya walimu (staff room) wa Shule ya Msingi Silabu iliyopo Wilaya ya Korogwe. dev.kisakuzi.com imelazimika kuitembelea tena shule hii ikiwa ni miezi sita baada ya kuitembelea awali mapema mwezi Agosti 2012.

Hili ni darasa jipya lililojengwa sasa katika Shule ya Msingi Silabu iliyopo Wilaya ya Korogwe, darasa hili linatumiwa na wanafunzi wa darasa la tatu. Lakini nje kivuli chake wakati wa jua kali ni ofisi ya walimu wa shule hiyo.

Madawati haya mbele ya darasa hili ni Ofisi ya walimu (staff room) katika Shule ya Msingi Silabu, husogezwa hapa baada ya kivuli cha mti kutoweka katika mti ambao hutumika kama ofisi shileni hapo.

Uchochoro huu awali ndio ulitumika kama darasa la tatu kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Silabu iliyopo Wilaya ya Korogwe. Jitihada za Serikali zimefanywa na sasa limejengwa darasa moja ambalo linatumiwa na wanafunzi wa darasa la tatu. dev.kisakuzi.com imelazimika kuitembelea shule hii tena ikiwa ni baada ya kipindi cha miezi sita. Awali (Agosti 2012) iliripoti wanafunzi wa darasa la tatu kusomea uchochoroni baada ya kutokuwa na darasa.

Choo hiki cha Shule ya Msingi Silabu kiliezuliwa na upepo muda mrefu sasa lakini kutokana na hali ngumu ya bajeti ya fedha bado hakijarekebishwa, Serikali inafanya juu chini kufanikisha hili itakapopata fungu la kutosha.