wadau wa Afya Australia Waipa Tanzania Magari ya Kubebea Wagonjwa

Muuguzi Mkuu wa Idara ya Afya kutoka Serikali ya Australia Bi. Catherine Stoddart (kushoto) akimkabidhi funguo za magari ya kubebea wagonjwa Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi.Regina Kikuli katika viwanja vya wizara hiyo jijini Dar es Salaam. Magari hayo mawili yaliyotolewa kwa msaada wa wadau wa afya wa mashirika yasiyo ya kiserikali ya Austaralia yatapelekwa kusaidia utoaji wa huduma za afya ya mama na mtoto katika hospitali ya Wilaya ya Kisarawe.

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Bi.Regina Kikuli akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya kupokea msaada wa magari 2 ya kubebea wagonjwa kutoka kwa wadau wa afya wa Australia.

Katibu mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi.Regina Kikuli(kulia) akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) funguo za magari mawili ya kubebea wagonjwa aliyokabidhiwa na wadau wa mashirika yasiyo ya serikali kutoka Austaralia. Picha zote na Aron Msigwa – MAELEZO.