Uzinduzi wa Mpango wa ‘Malaria Safe’

Wadau makampuni na taasisi mbalimbali wanaopambana na ugonjwa wa malaria nchini wakiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda baada ya uzinduzi wa ‘Malaria Safe Campaign’
mara

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda akimkabidhi cheti Mzee CHrisant Mzindakaya Mwenyekiti wa Kampuni ya Kuzalisha nyama ya mkoani Rukwa kwa mchango wake katika kupambana na Malaria nchini.

WIZARA ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na Kampeni ya Tuungane Kutokomeza Malaria, Unite against malaria (UAM) inaendeleza mapambano dhidi ya malaria kwa kuanzisha mpango wa kuzishirikisha kapuni na taasisi binafsi za hapa nchini ili ziwe mstari wa mbele katika mapambanoi dhidi ya malaria kwa kuwakinga na kuwapatia tiba sahihi wafan ya kazi wao, mpango huu unajulikana kama malaria safe program.
Mpango wa safe malaria ulizinduliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mzingo Pinda.Novemba 29, 2012 katika ukumbi wa kibo, Hyatt Regency – Kilimanjaro hoteli
Malengo ya mpango
 Kushirikisha makampuni binafsi katika mapambano dhidi ya malaria kwa kuhakikisha kuwa wafanyakazi wao pamoja na familia zao wanajikinga na malaria na kupata tiba sahihi ya malaria pale wanapougua.
 Kutoa elimu ya kujikinga na malaria kwa wafanyakzai na familia zao kwa kuhimiza matumizi ya vyandarua vyenye viwatilifu.
 Kuwa mawakala wa mapambano dhidi ya malaria kwa kuchngia katika uhamasishaji wa upatikanaji wa rasilimali ili kuendeleza mapambano dhidi ya malaria nchini.

Mpango huu pia unalenga katika kuchangia maeneo yenye mapungufu ya rasilimali fedha, katika kutoa kinga na tiba sahihi ya malaria nchini, ili kuweza kufikia malengo yaliyowekwa na serikali katika kuboresha afya za watanzania na hivyo kuchangia katika kuimmarisha utoaji huduma za afya kwa mapambano dhidi ya malaria nchini.
Makampuni binafsi ambayo yamejiunga na mpango huu wa malaria safe na yapo tayari kuelekeza nguvu zao katika apambano dhidi ya malaria hapa nchini yatatunukiwa cheti cha utambuzi (certificate of recognition) ambacho kitatolewa na mgeni rasmi wa uzinduzi.
Ukubwa wa tatizo la ugonjwa wa malaria unatammbulika dunia nzima, hapa nchini kutokana na takwimu ,inakadiriwa takribani watu milioni 10 hadi milioni 12 wanaugua malaria kila mwaka, na malaria husababisha vifo vya watu kati ya 100,000 hadi 300,000 kila mwaka. Aidha zaidi ya asilimia 40 ya wagonjwa wanaohudhuria katika vituo vya kutolea huduma za afya wanasumbuliwa na ugonjwa wa malaria.
Katika kudhibiti ugonjwa wa malaria serikali kupitia wizara ya afya na ustawi wa jamii inatekeleza mikakati inayolenga katika kuboresha kinga na tiba sahihi ya ugonjwa wa malaria.
Kwa upande wa kinga, umiliki (ownership) wa vyandarua vyenye viwatilifu vya muda mrefu ueongezeka katika miaka mitano iliyopita , na kufikia asilimia 91 na hii imetokana na kampeni mbalibali za ugawaji wa vyandarua zilizofanyika hapa nchini.
Kampeni hizo ni pamoja na ugawaji vyandarua kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano,upatikanaji wa vyandarua kwa wanamama wajawazito kupitia mpango wa hati punguzo na ugawaji wavyandarua kwa wananchi wote kwa ujumla sehemu za malazi katika kaya kupitia kampeni ya ugawaji wa vyandarua katika sehemu za malazi.
Njia nyingine za kinga ni upuliziaji wa dawa ukoko katika kuta ndani ya nyumba (indoor residual spraying)IRS, zoezi ambalo linaendelea katikia mikoa mitatu ya kanda ya ziwa;kagera,mwanza na mara, na mradi wa kuangamiza viluwiluwi vya mbu katika mazalia(Larviciding) zoezi ambalo linatekelezwa katikia mkoa wa Dar es Salaam.
Kadharika tiba ya malaria ,imeboreshwa kwa kuhakikisha kuwa tiba sahihi ya malaria kwa kutumia dawa mseto inapatikana katika vituo vya kutolea huduma za afya na sekta binafsi kwa bei ya punguzo. kwa upande wa upimaji wa vimelea vya malaria,sambamba na matumizi ya hadubini (microscope) pia matumizi ya kipimo cha utambuzi wa vimelea vya malaria kwa haraka (malaria rapid diagnosis tests-Mrdts, yanaendelea baada ya kukamilika kwa mafunzo kwa watoa huduma nchi nzima.
Mafanikio yanaonekana, kutokana na mikakati iliyoanishwa hapo juu, takwimu za utafiti wa vishiria vya malaria na virusi vya ukimwi )Tanzania HIV/AIDS na malaria indicators survey 2011/2012 zilizotolew hivi karibuni zinaonesha kuwa maambukizi/uwepo wa vimelea vya malaria kwa watoto chini ya miaka mitatno umepungua kwa asilimia 45 kutoka asilimia 18 kwa mwaka 2007/2008 kufikia asilimia 10 kwa mwaka 2011/2012.
Hata hivyo bado zipo changamoto mbalimbali katika mapambano dhidi ya malaria hapa nchini, kutokana na takwimu kutoka katika vituo vya huduma, malaria bado inaongoza katika matukio ya ugonjwa na vifo.pia malaria inaleta changamoto katika uzalishaji mali na hivyo kuchangia katika athari za kiuchui na hatimmaye maendeleo ya nchi kwa ujumla.
Kwa kushirikisha kampuni binafsi katika mapambano dhidi ya malaria, tunaamini itasaidia katika kupunguza athari za malaria kwa jamii na kwa nchi, kujiunga na mpoango wa malaria safe,makampuni yatatekeleza mambo manne muhimu.

1. Elimu;kukubali kueliisha wafanyakazi wake juu ya athari na tiba sahihi ya malaria
2. .Kinga ;kuwakinga wafanyakazi wake kwa kuhakikisha wanatumia vyandarua vyenye viwatilifu vya muda mrefu.
3. Muonekano; kuweka ujumbe wa malaria katika huduma wanazotoa/wanazozalisha.
4. .Utetezi; kukubali kuwa balozi wa kutetea mapambano dhidi ya malaria na kuhamasisha makampuni mengine kujiunga na mpangfo huo.
Serikali ya Tanzania inawajibu wa kiuhakikisha kwamba mikakati ya kupambana na malaria inakuwa endelevu kwa kushirikiana na sekta binafsi pamoja na wadau wengine wa malaria. Mpango huu wa malaria safe,utakuwa ni moja kati ya chachu za kuhamasisha utekelezaji wa mikakati ya kudhibiti malaria na hivyo kuchangia kupungua kwa ugonjwa wa malaria na hatimaye kuitokomeza kabisa.
Kwa pamoja tuungane kuitokomeza malaria
Malaria Haikubaliki- Tushirikiane kuitokomeza

Regina Kivuli
Kaimu Katibu Mkuu
Wizara ya afya na usitawi wa jamii.