Mhariri wa dev.kisakuzi.com akichanja mbuga na kupanda milima kuangalia maisha ya jamii za vijijini Korogwe juzi
Sehemu kubwa ya ardhi eneo hili la Korogwe Vijinini ni milima na barabara zimechongwa pembeni ya milima.
Mashamba ya zao la chai Kijiji cha Bungu Msigwa Korogwe Vijijini
Mashamba ya zao la chai Ifune, Korogwe vijijini. Kwa mujibu wa maelezo ya wakulima kilo moja ya zao la chai wanauza kwa sh 200. Kilio chao kikubwa ni kupata Kiwanda chao kitakacho inua kipato chao kwani hivi sasa wanakandamizwa kibei.
Miti hii hukatwa na kutumika kukaushia zao la chai na wawekezaji wa chai eneo hilo.
Sehemu kubwa ya ardhi ya Korogwe Vijijini ni Milima na miinuko lakini hali hiyo haizuii kupata viwanja vya michezo chapokuwa si tambalale kama ilivyo kwa maeneo mengine. Pichani wanafunzi wa Shule ya Msingi Bungu wakicheza kabumbu wakati wa mapumziko.
Hii ndio hali ya hewa eneo la Kijiji cha Bungu Korogwe Vijijini nyakati za asubuhi, ni ukungu wa baridi kama ulaya vile.
Mjumuiko huu ulikutwa pembezoni mwa barabara lakini mazungumzo yao yote yalikuwa kwa lugha ya kisambaa, haijalishi wewe unajua au la..! “Speak Kisambaa”
Katika safari hiyo niliongozana na mwanahabari mwandamizi Elizabeth Mjatta (kushoto)kutoka kampuni ya New Habari (2006), wachapishaji wa magazeti ya Mtanzania, Rai na The Arican na hapa alikuwa akipata picha na baadhi ya wanakijiji waliotupokea Kijiji cha Bungu.
Asante usafiri huu kwa kutupandisha milima kutoka kijiji kimoja hadi kingine. Hapa Elizabeth Mjatta akipata picha ya kumbukumbu. Picha zaidi baadaye