Peer Educators wa kampuni ya CFAO MOTORS Grasiano Mfuse (katikati) na Maria Petro wakikabidhi msaada wa chakula, mafuta na maziwa kwa Mwenyekiti wa TMH Bi. Khadija Mwanamboka kwa ajili ya watoto wa kituo cha Tanzania Mitindo House ambao miongoni mwao wanaishi na Virusi vya Ukimwi.
Pichani juu na chini ni Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Kituo cha Watoto yatima wa Tanzania Mitindo House (TMH) Bi. Khadija Mwanamboka akitoa shukrani kwa Ujumbe wa CFAO MOTORS kwa kutambua mchango wake katika jitihada zake za kulea watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu.
Wanafunzi na Ujumbe wa CFAO MOTORS ndani ya Chumba cha darasa la THM kilichopambwa na kuwekwa Samani na Kampuni hiyo Ujumbe wa CFAO Motors wakitizama ufanisi wa kazi za mikono zinazofanywa na watoto yatima wa vituo mbalimbali waliokusanyika kupata mafunzo ya ufundi bure katika shule ya Tanzania Mitindo House. Kulia Meneja Masoko wa CFAO MOTORS Bi. Tharaia Ahmed na Peer Educators kutoka kampuni hiyo Bw. Grasiano Mfuse (kushoto) na Maria Petro (katikati).
Mwalimu wa Darasa la TMH la watoto yatima wa vituo mbalimbali la Tanzania Mitindo House Dkt. Linda August akiwafundisha mabinti kutengeneza baadhi ya bidhaa za urembo kama mikufu na hereni kwa kutumia shanga.