Semina Juu ya Ustawi wa Mwajiriwa

Baadhi ya Washiriki wa Semina Juu ya Ustawi wa Mwajiriwa wakifuatilia semina hiyo.

Mtaalamu wa Ustawi wa mwajiriwa Bw. Doug Bramsem akitoa somo katika semina juu ya Ustawi wa Mwajiriwa iliyofanyika hoteli ya Sea Cliff jijini Dar es Salaam. Semina hiyo ilikuwa na lengo la kuwawezesha washiriki kujua nini maana ya Ustawi wa Mwajiriwa, jinsi ya kuendesha kampuni na kupata faida na kujua historia ya Ustawi wa Mwajiriwa nchini Tanzania na kumjenga mfanyakaziwako kuwa bora na kutatua ustawi wake katika kampuni zao
 Mtaalamu wa Ustawi wa mwajiriwa Bw. Doug Bramsem akikazia neno.

Mtaalamu wa magonjwa ya akili kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha magonjwa ya akili, Prof. Gad Kilonzo akizungumzia Ustawi wa Mwajiriwa.
 Mtaalamu wa mambo ya Saikolojia, Bi. Lisa Finke kutoka GIZ akitoa somo katika semina hiyo.
 Mtaalamu wa Ustawi wa mwajiriwa, Dk. Hilde Basstanie kutoka GIN akitoa somo la ugonjwa wa Ukimwi jinsi ya kujilinda makazini.
 Washikiri wakifuatilia kwa makini semina hiyo.
Mmoja ya washiriki wa semina hiyo, Bw. James Lwanga kutoka hospitali ya Kadic iliyopo Bukoto, Uganda akielezea mambo mbali mbali yanayofanyika katika jamii nchini kwao.
 Washiriki wakifuatilia kwa makini semina.
  Mtaalamu wa Ustawi wa mwajiriwa,  Dk. Hilde Basstanie (kwanza kulia) kutoka GIN akiwa na washiriki wengine wakifuatilia kwa makini.
Washiriki wakiwa makini kupata somo.