MTANDAO wa Jinsia Tanzania kwa kushirikiana na wamekuwawakifanya kazi kubwa sana ya kupinga ukatili wa kijinsia hasa ukatili dhidi ya wanawake duniani. Kampeni ya Siku 16 za Kupinga Unyanyasaji wa jinsia imetumika kama jukwaa mahsusi, kujenga uelewa kuhusu ukatili wa kijinsia kama ukiukaji wa haki za binadamu kijamii, kitaifa, kikanda na kimataifa. Pia kuimarisha kazi za kupinga ukatili dhidi ya wanawake katika ngazi za kijamii na kujenga daraja kati ya maeneo mbalimbali yanayoshughulikia ukatili dhidi ya wanawake.
Kauli mbiu ya siku hii kitaifa ni ”Funguka kemea ukatili dhidi ya wanawake; sote tuwajibike”.
Kwa mwaka huu, TGNP itaadhimisha Kampeni ya Siku 16 za kupinga unyanyasaji wa Kijinsia siku ya Jumaatano tarehe 28 Novemba 2012 katika viwanja vya Mtandao wa Jinsia Tanzania Mabibo kuanzia saa 3.00 asubuhi mpaka saa 8.00 Mchana .Washiriki kutoka maeneo mbalimbali wkiwemo wanaharakati/mitandao, vikundi vya wanaharakati katika ngazi ya jamii, asasi za kiraia vyama vya wafanyakazi, asasi za kidini, taasisi za elimu, taasisi za serikali, taasisi za kimataifa na ofisi za ubalozi wanatarajiwa kushiriki.
Kwa kuzingatia mchango wa taasisi/asasi/ofisi yako katika utetezi wa haki na usawa kijinsia, waandaaji wanakualika kuwa mmoja wa washiriki katika maadhimisho haya. Tafadhali thibitisha ushiriki wako kupitia barua pepe