Wabunge ‘kumsulubu’ Mkulo Dodoma leo

Baadhi ya wabunge wakiwa bungeni Dodoma.

Na Mwandishi wa Thehabari, Dodoma

WABUNGE leo wanatarajia kuendelea na vikao vya Bunge baada ya Spika Anne Makinda kuhairisha vikao kwa mapumziko ya mwishoni mwa wiki huku baadhi ya wabunge wakisubiri kwa hamu kuichambua bajeti ya mwaka 2011/2012 iliyowasilishwa na Waziri wa Fedha na Uchumi Mustafa Mkulo.

Kabla ya wabunge hao kumpzika, Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo alisoma
bajeti ya Serikali kwa mwaka 2011/2012 ambapo sasa wabunge hao wataanza
kuichambua kuanzia Jumatano wiki hii.

Kwa mujibu wa ratiba ya Bunge, leo wabunge wanatarajia kuanza kujadili kwa kina Mpango wa Miaka Mitano wa Maendeleo ambao ulizinduliwa rasmi na Rais Jakaya kikwete mjini hapa.
Katika kuijadili huko pamoja na mambo mengine wabunge wataweka mikakati
na malengo ambayo itawezesha kufanikiwa kwa mpango huo ambao unalenga kuleta maendeleo ya nchi na watu wake.

Wakati Makinda anaahirisha Bunge hilo aliweka wazi kuwa siku mbili ili waweze kuusoma mpango huo na hata watakapokuwa wanachangia wasiwe hawana uelewa wa kutosha kwani matokeo yake watashindwa kueleweka kwa wananchi wanafuatilia Bunge.

Wabunge wataanza na kipindi cha maswali na majibu asubuhi na kufuatiwa na mjadala BUNGE linatarajia kuendelea na vikao vyake leo mjini hapa baada ya kuahirishwa mwishoni mwa wiki iliyopita.

Baada ya kumaliza kujadiliwa kwa mpango huo wa maendeleo, Bunge linatarajiwa kuwa la moto zaidi wakati wa kuchangia bajeti ya mwaka 2011/2012 ambayo imewasiliwa na Mkulo ambapo baadhi yao wameahidi kuichambua kwa kina na kuelezea mabaya na mazuri ya bajeti hiyo.

Ni wazi kuwa tangu kusomwa kwa bajeti hiyo tayari mijadala katika maeneo mbalimbali imekuwa ikiendelea kwa wananchi kutoa maoni yao kuhusu bajeti hiyo ambayo wengi wameipongeza kuwa inagusa maisha ya wananchi wote na hasa wanyonge.

Mbali ya wabunge kuichambua bajeti hiyo, Kambi ya Upinzani Bungeni kupitia Waziri kivuli wa Fedha Zitto Kabwe ambaye pia nia Msemaji wa kambi hiyo, itawawasilisha bajeti mbadala ambayo wanaamini ndio mkombozi kwa wananchi.

Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe baada ya Mkulo kusoma bajeti yake ya mwaka 2011/2012 Jumatano iliyopita, aliisifu kuwa ni nzuri lakini akaweka wazi bajeti ya wapinzani itakuwa nzuri zaidi na ndio inayoweza kumsaidia mwananchi.

Ratiba ya vikao vya Bunge la Bajeti inaonesha kuwa Juni 22 mwaka huu, Muswada wa Sheria ya Fedha utawasilishwa na kuanzia Juni 23 wizara mbalimbali za Serikali zitaanza kuwasilisha hotuba za bajeti za wizara hizo kupitia mawaziri wao.

Hata hivyo kiu ya Watanzania walio wengi wanasubiri kwa hamu kubwa bajeti ya Wizara ya Utumishi wa Umma ambayo itatangaza nyongeza ya mshahara kwa maana ya kima cha chini kwa watumishi wa umma.

Waziri Mkulo wakati anazungumza na waandishi wahabari, mjini hapa , alisema kuwa wakati anasoma bajeti hiyo aligusia suala la mishahara lakini hakutaja kima cha chini kwasababu ya utaratibu na kwamba atakayezungumzia hilo nia waziri mwenye dhamana ya watumishi wa umma.