Barrick Yapewa Tuzo na PPF


Kampuni ya uchimbaji madini ya African Barrick Gold (ABG) kupitia mgodi wake wa dhahabu wa Bulyanhulu uliopo wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga imepewa tuzo ya mwaka 2012 na mfuko wa pensheni wa PPF baada ya kuibuka mshindi wa kwanza kwenye sekta ya madini kwa ulipaji mzuri wa michango ya wafanyakazi kwa muda. Kwenye picha ni Meneja Rasilimali Watu na Utawala wa ABG, Saimon Sanga, akiwa ameshika kikombe na cheti ambavyo ABG ilikabidhiwa na PPF hivi karibuni. PICHA/MPIGA PICHA WETU.