Uwepo wa Serikali Mbili Ndio Sera Sahihi ya CCM – Dk. Shein

Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, (katikati) akisalimiana Umati Mkubwa wa Wananchi nna wanaCCM waliofika kwa mapokezi yake katika Viwanja vya CCM KIsiwandui Mjini Zanzibar akitokea Dodoma katika Mkutano Mkuu na Uchaguzi wa Viongozi wa juu katika chama hicho cha CCM.(Picha zote na Ramadhan Othman,Ikulu)

Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk. shein akiingia uwanjani. Kulia ni Katibu Mkuu wa chama hicho taifa, Abdulrahman Kinana. Watatu kulia ni Vuai Ali Vuai

Mamia ya wana-CCM Uwanja wa Kibandamaiti

Na Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuwa kuwepo kwa Serikali mbili ndio sera sahihi ya CCM, na kusisitiza kuwa umoja ndio nguzo itakayokipa ushindi chama hicho katika chaguzi zake zote zijazo. Hayo aliyasema katika mkutano wa hadhara wa Wana-CCM na wananchi wa mikoa ya Unguja, uliofanyika huko katika uwanja wa Demokrasia, Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa CCM wa Tanzania Bara na Zanzibar.

Alisisitiza kuwa Malengo ya Mapinduzi yatalindwa na kutunzwa pamoja na kuyaendeleza huku akisisitiza kuwatumikia Wazanzibari wote na kuondokana na ubaguzi wa rangi kwa lengo lile lile la Mapinduzi. Mapinduzi hayo ndio yaliokuwa Dira ya kuanzisha CCM, na kueleza kuwa waasisi akiwemo Marehemu Mzee Karume na Julius Kambarage Nyerere na kueleza kuhusi muungano na kusisitiza kuwa waasisi hao wataendelea kutunzwa na kufuatwa yazyo zao.

“Sisi CCM, tuna chama chetu na wao wana vyama vyao, sisi tuna sera zetu na wao wana sera zao, kila mmoja anahubiri sera zake, hatujaunganisha vyama hata siku moja na wala hatutounganisha vyama hata siku moja”,alisisitiza Dk. Shein.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimia baadhi ya viongozi wa CCM, baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Zanzibar, kwa ajili ya kushiriki sherehe za kupongezwa safu mpya ya uongozi wa CCM Kitaifa, uliopatikana mjini Dodoma, zinazofanyika leo Viwanja vya Demokrasia (KibandaMaiti) mjini Zanzibar. Wengine ni Wajumbe wa Sekretarieti mpya ya CCM, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai, Naibu Katibu Mkuu (Bara) Mwigulu Nchemba na Katibu wa NRC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.(Picha na Bashir Nkoromo)

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akivishwa Skafu na Chipukizi wa CCM, baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Zanzibar, kwa ajili ya kushiriki sherehe za kupongezwa safu mpya ya uongozi wa CCM Kitaifa, uliopatikana mjini Dodoma, zinazofanyika leo Viwanja vya Demokrasia (KibandaMaiti) mjini Zanzibar. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Nchemba na Watatu ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Zanzibar Vuai Ali Vuai. (Picha na Bashir Nkoromo)

Alisema kuwa kila chama kinahuribi sera zake na CCM itaendelea kuhubiri siasa za kistaarabu bila ya kuhubudhiana. “ na uchaguzi mkuu tutashindana na CCM itashinda. CCM ina wafuasi wengi na inaungwa mkono na wananchi wengi na Muungano utadumu”,alisema Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar.

Alieleza kuwa nchi nyingi katika bara la Afrika zilijaribu kutaka kuunda Muungano kama ilivyofanya Tanzania lakini walishindwa. Alieleza kuwa katika sekta mbali mbali za maendeleo kumekuwepo kwa mashinrikano makubwa ndani ya Muungano ambapo faida hupatikana kwa wote na kusema kuwa Muungano huo una faida kubwa hasa za kibiashara.

Alieleza kuwa wafany biashara wengi wanafanya biashahara Tanzania Bara na wengi wao wanaishi Tanzania Bara, “Muungano huu ni bora kuliko wote na ule wa Mkataba sisi hatuujui”. Sisi tumezoea Muungano wa Serikal”,alisema Dk. Shein.

Makatibu wa NEC, Mohamed Seif Khatib (Oganaizesheni na Asha-Rose Migiro (Siasa na Mambo ya Nje) wakiteta jambo wakati wa mkutano wa wana-CCM Zanzibar kuipongeza safu mpya ya uongozi wa CCM Taifa, kwenye viwanja vya Kibandamaiti, mkoa wa mjini

Viajana wa CCM wakishangilia kwa mtindo wa aina yake

Akieleza kuhusu utoaji maoni wa mabadiliko ya Katiba ya Jamhutri ya Muungano Dk. Shein alisema kuwa hatua iliyopo hivi sasa ni ya mwanzo tu na inatoa fursa kwa kila mmoja kutoa maoni yake. Aliwataka wananchi na WanaCCM, kwenda kutoa maoni. Alieleza kuwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, itadumishwa na kuendelezwa kwa lengo la kuleta mustakbali wa wananchi wote na kueleza kuwa madhumuni yake ni lkulea maendeleo bila ya kubudhubdiana tena bila ya kugombana.

“Mimi ndio rais wa Serikali hii”, wanaofanya vituko mimi nawanyari ninawaperemba kama ubwabwa wa Pemba, niko imara niko makini kuiomngoza Zanzibar, siongozi kwa kubahaishwa, naongoza kwa taratibu zote ziliopo…Serikali hii yetu sote na mimi ndio rais wake nilioshika usukani”, alisema.

Akieleza kuhusu amani na utulivu na kusisitiza kuwa jambo hilo halina mbadala na itaendelea kutunzwa na hatomvumilia yeyote atakae vuruga amani na utulivu uliopo nchini.“Sitomvumilia ataekae vuruga amani”alisema.

Alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar haitoweza kuzuia shughuli za dini zisifanyike na hatozuiliwa mtu kuabudu, na kueleza kuwa lakini mtu au kikundi cha watu wasisingizie dini kuvuruga amani kwani sheria na taratibu zitawaandama.

Alitoa pongezi kwa vyombo vya ulinzi na usalama, katika kurudisha amani kwa kutumia taratibu na sheria, na kusisitiza kuwa amani iliyopo isichezewe huku akisema kuwa ana imani kubwa na vikosi hivyo yeye na Mwenyekiti wa CCM Dk. Jakaya Mrisho Kikwete.

“Hatuwezi kuwaachia wachache kuvuruga amani”,alisema. Na kueleza kuwa serikali zote mbili zitahakikisha kuwa hakuna anaebughudhiwa na kunyanyaswa. “Nimekuwa kiapo pale amani kuwa nitaingoza Zanzibar kwa kuwatendea haki wananchi wote”alisisitiza.

Alisisitiza kuwa kuna haja ya kuyaendeleza na kuyalinda majimbo yote ya uchaguzi nay ale yaliochukuliwa na upinzani ni lazima yarejeshwe kwa nguvu zote. Alitaka kuhakikisha kuwa maskani zinaimarishwa na zote zilizosinzia ziimarishwe,na kusema kuwa vuguvugu za maskani lazima ziwepo.

“Ushindi wa 2015 sasa maandalizi yake yako tayari, CCM sio chama cha mchezo”,alisema Dk. Shein.

Nae Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai, alitoa salamu za Komandoo Dk. Salmin Amour Juma Rais mstaafu wa Zanzibar ambazo zilieleza kuwa yeye yuko pamoja na wanaCCM katika kumtakia kila la heri Makamu Mwenyekiti mpya wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein. Katika risala ya wanachama wa CCM wa Mikoa ya Zanzibar walieleza kuwa ushindi alioupata Dk. Shein wa asilimia mia moja unatokana na juhudi zake za kuleta maendeleo nchini.

Risala hiyo pi,a iliwapongeza viongozi wote wa Halmashauri Kuu ya CCM pamoja na Kamati ya Sektarieti ya CCM.
Ilieleza kuwa uwezo alionao Dk. Shein ni thibitisho kubwa la mafanikio kwani lengo kuu ni kumaliza siasa za chuki na kuleta amani na utulivu licha ya kujitokeza baadhi ya vikundi ambavyo vinataka kuvuruga amani hiyo iliyopo nchini.

Risala hiyo ilieleza kuwa vikundi hivyo vilihatarisha amani ya Zanzibar ambayo ina historia kubwa kwa kuvuruga amani na kuleta vurugu kwa kuharibu mali za wananchi pamoja na Serikali, majengo ya CCM, nyumba za ibada yakiwemo Mkanisa na kusababisha hasara ya mamilioni ya fedha. Waliwasihi Wazanzibari na Watanzania wote juu ya kuendeleza na kuidumisha amani na mshikamano uliopo, ambao ndio siri kubwa ya mafanikio na maendeleo yaliopo, na kulani kwa nguvu zote kitendo cha kumwagiwa tindi kali kwa Katibu wa Mufti wa Zanzibar Sheikh Soraga.

Walieleza kuwa watu waovu hawakupenda kumuona Sheikh Soraga akihubiri amani, na kuviaomba vyombo ya dola kuwatafuta wale wote waliohusika na tukio hilo na kueleza kuwa wanaCCM wanalaani kwa nguvu zote tukio hilo.