Kilaini Akana Kuzungumza na Gazeti la Mwananchi na Kuponda Viongozi wa CCM

Askofu Method Kilaini

LEO katika moja ya habari zake gazeti la Mwananchi limemnukuu Askofu Msaidizi wa Jimbo la Bukoba, Method Kilaini kuuponda uteuzi wa sekretarieti mpya ya CCM iliyoteuliwa juzi Dodoma. Kauli ya askofu huyo ameituma kwa vyombo vya habari akipinga kuzungumza na gazeti hilo. Soma kauli yake hapo chini;

“TAMKO – STATEMENT

Kwa masikitiko makubwa nimesoma katika gazeti la Mwananchi kwamba nimeiponda safu ya uongozi na sekretariati ya CCM. Mimi sijaongea na gazeti lolote juu ya uongozi wa CCM na wala sina nia au sababu ya kuuponda uongozi huo. Ni vibaya kwa gazeti lo lote lile kutumia jina la mtu kwa kueneza maoni yake. Kama ni waugwana natumaini watasahihisha waliyoyaandika. Nasikitika sana kwa walikwazwa na hilo. Askofu Kilaini” hii ni taarifa yake fupi Kilaini.

Askofu Method Kilaini

Bukoba Catholic Diocese

e-mail: mkilaini@gmail.com

Web: http://bukobadiocese.catholicweb.com

http://card-rugambwa.catholicweb.com