BONDIA Baina Mazola toka katika gym ya Mzazi Respect ya Mabibo atazipiga na mtoto wa Mwananyamala, Mwaite Juma katika pambano lisilo la ubingwa la raundi nane. Pambano hilo litafanyika Jumapili ya Novemba 18, 2012 katika Ukumbi wa DID Mabibo, ambalo ni maalumu kuwania kucheza ubingwa huo. Mshindi wa pambano hilo atakuwa na nafasi ya kucheza pambano la ubingwa na bondia bingwa wa uzito huo.
Pambano hilo lililoandaliwa na kuratibiwa na Christopher Mzazi, pia litakuwa na michezo mingine yenye lengo la kunyanyua vipaji vya mabondia chipukizi ambao wamekuwa na upinzani na uhasama toka sehemu mbalimbali ili wamalize kiu zao, kwani kuna baadhi ya vijana hao kuna waliofikia kupigana mitaani na wengine kurushiana maneno makali na kutishiana kuwa kila mmoja mbabe kwa mwenzake.
hivyo wameandaliwa pambano wamalize bifu na kiu zao ili waendelee na mchezo kama mchezo kwa kunyanyua na kuendeleza vipaji vyao kwa manufaa yao kama ajira na maendeleo kwa taifa. Katibu mkuu wa ngumi za kulipwa nchini IBRAHIM KAMWE amethibitisha kuwepo kwa pambano hilo na taratibu zote za mchezo wa ngumi zipo katika hatua ya mwisho kukamilikaa na mapambano ya utangulizi yatakuwa kama inavyoonesha hapo chini.
Mapambano mengine ni;
light fly – HERMAN SHEKIVULI V/S OMAR MAKUSUDI 4round
light fly – MARTIN RICHARD SHEKIVULI V/S SHOMARI PENDEZA 4round
light fly – ISSA OMAR V/S JAMES MARTIN 6round
wealter weight – ABDALAH LUWANJE V/S SAID MUHIDIN 6 round
light weight – mpole mackenzie v/s Adam Barnaba. 4 round
super fly – Shadrack juma v/s Ramadhan ustadh 4 round
Ngoyi Gaudence v/s Idd Mbishi 4 round