JUMUIYA ya watumiaji wa huduma mbalimbali nchini kupitia mitandao ya kijamii ya Facebook na Twitter imezindua rasmi shindano la kusaka kampuni zinazotoa huduma na bidhaa mbovu kwa wateja nchini Tanzania. Jumuiya hiyo inawajumuisha watu wa kada mbalimbali wakiwemo wanasheria, wanaharakati, waandishi wa habari, viongozi wa kisiasa, wafanyabiashara na wateja wa huduma na bidhaa mbalimbali nchini Tanzania.
Lengo la jumuiya hiyo ni kushinikiza wafanyabiashara nchini kutoa huduma na bidhaa bora kwa wateja na kuwakumbusha umuhimu wa wateja. Kauli mbiu ya wanajumuiya hao ni Mteja ni Mfalme. Katika wiki ya kwanza tangu jumuiya hiyo kuzinduliwa jumla ya makampuni 21 yameingizwa katika shindano hilo kwa wateja wao kuwasilisha malalamiko yao. Kwa taarifa zaidi kuhusu ni fuatilia akaunti ya Twitter @hudumambayatz au kundi la Facebook linalojulikana kama HUDUMA BONGO.
Ili kuweza kupiga kura yako unahitajika kuwa na akaunti hai (yenye mawasiliano mara kwa mara) katika mtandao wa Twitter au Facebook na kujiunga na jumuiya hiyo. Mara tu utakapowasilisha kero yako utaifanya kampuni unayoilalamikia kuingia katika mchuano mkali wa kumsaka bingwa wa huduma mbovu kwa wateja nchini.
Huduma Bongo inatoa wito kwa makampuni yote kuboresha huduma na bidhaa zao ili kuweza kuwapatia wateja kilicho bora zaidi katika soko hili la ushindani. Imetolewa na Mshauri wa Habari wa Huduma Bongo – hudumabongo@gmail.com