Mhasibu TGNP Afariki Dunia

Nembo ya TGNP

Tunasikitika kuwapa taarifa kwamba ndugu Claudian Raphael Ndayi aliyekuwa ameajiriwa na TGNP kama Mhasibu alifariki tarehe 5 November 2012 katika hospitali ya Agakhan. Mipango ya kumwaga itakuwa kama ifuatavyo:

Jumatano Tarehe 7 Novemba 2012 mwili wa marehemu utapelekwa nyumbani kwake Kibada kigamboni na kutakuwa na mkeshaAlhamisi Tarehe 8 Novemba 2012 kuanzia saa 4.00 asubuhi kutakuwa na Ibada na heshima za mwisho zitatolewa nyumbani kwake na baada ya hapo kutakuwa na msafara kwenda Airport ambapo mwili wa marehemu utasafirishwa kwenda kisiwa cha Kome, Sengerema – Mwanza

Kutakuwa na usafiri wa pamoja kwenda Kibada Kigamboni magari yataondoka kutoka hapa TGNP Saa 2.30 asubuhi. Kwa wale watakaotumia usafiri binafsi ifuatayo ni namna ya kufika nyumbani kwa Claudian:

Baada ya kuvuka Ferry unakwenda moja kwa moja barabara ya kwenda Mji Mwema ukifika njia panda ya kwenda Mji Mwema ingia kulia; kushoto kuna Petrol Station ya Oil Com. Baada ya hapo endesha moja kwa moja. Ukifika Kibada shule ya Msingi ambayo iko upande wa kulia mbele kidogo kuna mahali wanatengeneza matofari na kuuza vifaa vya ujenzi ( Mwafrika Hardware) utangia kulia na baada ya hapo kutakuwa na vibao vinavyotoa malekezo ya jinsi ya kufika kwa Claudian:

Dressing Code: Wafanyakazi tumeamua kuvaa T shirts za TGNP, yoyote ile GF 2011 au yoyote uliyo nayo. Members pamoja na Bodi kama mnazo Tshirts mnaweza kuvaa.

Pia tutakuwa na shairi ambalo tutaimba pamoja, tutaprint kila moja atakuwa na nakala likiwa tayari tutatuma pia soft copy.

Tunatanguliza shukrani.

Anna Kikwa
Head:Programme Support Management
Tannazia Gender Networking Programme
P.O.Box 8921
Dar es Salaam
Phone: 255 (0) 22 2433205/2443250
Mobnile: 0754 788 706/ 0715 788 706/6785 788 706