Bei ya Korosho Msimu Mpya 2012/2013 Sasa Sh. 1200

Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya korosho Tanzania Mudhihili Mudhihili (kushoto) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) makao makuu ya bodi hiyo jijini Dar es Salaam kuhusu bei ya mkulima ya kununulia korosho msimu wa 2012/2013 kuwa sh. 1200 kwa daraja la kwanza na 960 kwa daraja la pili. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Masoko wa bodi ya Korosho Tanzania Theofora Nyoni. Picha na Anna Nkinda – Maelezo


Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya korosho Tanzania Mudhihili Mudhihili (kulia) akiwaandikia waandishi wa habari jina lake wakati wa mkutano baina yao uliofanyika Makao Makuu ya Bodi hiyo jijini Dar es Salaam. Katika mkutano huo mambo mbalimbali yaliongelewa ikiwa ni pamoja na bei ya mkulima ya kununulia korosho msimu wa 2012/2013 kuwa sh. 1200 kwa daraja la kwanza na 960 kwa daraja la pili. Picha na Anna Nkinda – Maelezo