Luteni Jenerali Mstaafu Abdulrahman Shimbo akiingia kwenye gari lake aina ya Toyota landcruiser alilopewa zawadi na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambalo amelitumikia kwa zaidi ya miaka 41 akishika nyadhifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi. Sherehe za kumuaga zilizofanyika katika kambi ya Jeshi hilo Mgulani jijini Dar es Salaam. Picha na Anna Nkinda – Maelezo
Luteni Jenerali Mstaafu Abdulrahman Shimbo akikagua kikosi cha askari wa kike kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakati wa sherehe za kumuaga rasmi zilizofanyika katika kambi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Mgulani jijini Dar es Salaam. Luteni Jenerali Mstaafu Shimbo amelitumikia jeshi hilo kwa zaidi ya miaka 41 kwa kushika nyadhifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na mnadhimu mkuu wa Jeshi.
Mkuu wa Majeshi ya ulinzi nchini Jenerali Davis Mwamnyange akimkabidhi hati ya utumishi Luteni Jenerali Mstaafu Abdulrahman Shimbo (kushoto) wakati wa sherehe za kumuaga zilizofanyika katika kambi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Mgulani jijini Dar es Salaam. Luteni Jenerali Mstaafu Shimbo amelitumikia jeshi hilo kwa zaidi ya miaka 41 kwa kushika nyadhifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na mnadhimu mkuu wa Jeshi.
Luteni Jenerali Mstaafu Abdulrahman Shimbo (aliyesimama kwenye gari) akisindikizwa maafisa na askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ikiwa ni kuhitimisha sherehe za kumuaga rasmi zilizofanyika katika kambi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Mgulani jijini Dar es Salaam. Luteni Jenerali Mstaafu Shimbo amelitumikia jeshi hilo kwa zaidi ya miaka 41 kwa kushika nyadhifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na mnadhimu mkuu wa Jeshi.
Ndugu, jamaa na marafiki wa Luteni Jenerali Mstaafu Abdulrahman Shimbo (wanne mstari wa mbele kulia) wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa sherehe za kumuaga zilizofanyika katika kambi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Mgulani jijini Dar es Salaam. Wa katikati mstari wa mbele ni Mkuu wa Majeshi ya ulinzi nchini Jenerali Davis Mwamnyange. Picha zote na Anna Nkinda – Maelezo