BENDI kongwe ya muziki wa dansi Tanzania, Msondo Ngoma ‘Baba ya Muziki’ imetoa ratiba yao katika wiki baada ya kutoa burudani Dar es Salaam wiki iliyopita sasa wamerudi tena kwa ajiri ya kutoa burudani burudani nzuri zaidi wamesema kuwa wataanza kutoa burudani.
Siku ya Jumatano watakuwa ndani ya Ashok Pub-Mbagala Kuu, Alhamia watakuwa Ya Wipes Pub-Mivinjeni, Ijuma watakuwa katika bonanza, Lidaz Club-Kinondoni, Jumamosi Hii Watakuwa Kigamboni katika Ukumbi wa Mama’ Z & Papa ‘Z. na Jumapili watamaliza wiki end katika ukumbi wa Max Bar Ilala Bungoni. Akizungumzia ratiba hiyo Msemaji wa Msondo, Rajabu Mhamila alisema wameamua kutoa ratiba ili mashabiki wao waweze kujua nini kinaendelea baada ya ratiba ya awali kumalizika.
“Msondo ipo kamili katika kutoa burudan na ndiyo maana imeamua kutoa ratiba, hivyo tunaamini mashabiki wetu watakuja kwenye maonesho yetu kwani bila wao sisi hatuwezi kusimama na kuimba,” alisema.
Alitaja vibao vinavyotamba kwa sasa vya bendi hiyo kuwa na Suluhu wa Sabani Dede, Nadhiri ya Mapenzi wa Juma Katundu na Baba Kibene wa Eddo Sanga mbali na nyimbo hizo bendi hiyo itapiga nyimbo zake zilizotamba zamani zikiwemo Asha Mwanasefu, Cheusi Mangara, mwana Mkiwa na nyingine nyingi zilizotamba kipindi hicho.