Mbunge Joshua Nassari Akanusha Kufyatua Risasi Uchaguzi wa Madiwani Arusha

Mbunge wa Arumeru Mashariki (CHADEMA), Joshua Nassari

MBUNGE wa Arumeru Mashariki (CHADEMA), Joshua Nassari amekanusha taarifa zilizoandikwa na magazeti ya Uhuru na Habari Leo kuwa alifyatua risasi na kuzua tafrani katika uchaguzi wa kumtafuta Diwani wa Kata ya Daraja Mbili ya Jijini Arusha, uchaguzi uliofanyika jana ambapo mgombea wa Chadema aliibuka mshindi.

Nassari ameyasema hayo wakati akihutubia katika Mkutano wa hadhara kuzindua kampeni nyingine za chama chake kwa ajili ya chaguzi za Serikali za Mitaa kwa ajili ya Halmashauri ndogo ya Mji wa Usa River unaotarajiwa kufanyika Jumapili ijayo ya Novemba 4, 2012.

Mkutano huo ambao umehudhuriwa na watu wengi, umefanyika katika viwanja vya Ngaresero Usa-River ambapo mbali na Nassari, Katibu wa CHADEMA Kinondoni Ng Henry Kileo nae alikuwepo na alipewa nafasi ya kuzungumza.

Nassari amedai kuwa katika uchaguzi wa jana yeye alikuwa Wakala Mkuu wa CHADEMA Kata ya Bangata na hivyo kumhusiha na ya Daraja Mbili haelewi inakujaje. Amedai kuwa mtu aliyefyatua risasi ni Mwenyekiti wa UVCCM, Godwin Mwalusamba na kwamba Polisi walimuweka ndani na kuandika maelezo yake, lakini anashangaa kuambiwa ni yeye wakati siyo!

Akifafanua zaidi aliviomba vyombo vya usala avinavyohusika na maswala ya vibali vya kumiliki silaha za moto, kufanya uchunguzi wao na waeleze hiyo bunduki walimpa lini na ni risasi zimetumika, na kwamba kama ni kumkamata yeye yupo huru muda wowote wanaweza kumkamata.
Picha na Habari: arusha255.blogspot.com