Polisi Waua Watatu Mombasa, Kamanda “Gordon” auwawa Somalia

*Kamanda “Gordon” auwawa Somalia

POLISI nchini Kenya wakiri kuwauwa watu wawili wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa Kiislamu mjini Mombasa. Msemaji wa polisi alieleza kuwa watu hao waliuwawa katika mapambano ya risasi wakati polisi walipovamia nyumba moja. Alisema bastola, maguruneti na risasi zilikutikana kwenye nyumba hiyo. Kumetokea mapambano kadha mjini Mombasa katika miezi ya karibuni, baina ya Polisi na Waislamu.

Polisi nchini Kenya

KAMANDA mwanadamizi wa Somalia ameuwawa alipoviziwa na kushambuliwa na kundi la wapiganaji wa Kiislamu, Al Shabaab. Jeshi la Somalia na AMISOM waonyesha silaha walizopata kutoka al-Shabaa, Mogadishu. Gavana wa Jimbo la Shabelle Kusini, Kusini mwa Somalia, alisema Jenerali Ibrahim Mohamed Farah Gordon na wanajeshi wengine watatu waliuwawa karibu na mji wenye bandari, mji wa Merca.

Al Shabaab – ambao wanadhibiti eneo karibu lote la kusini na kati mwa Somalia – hivi karibuni waliondoka katika miji yote mikubwa, pamoja na Merca. Kundi hilo bado linafanya mashambulio ya kuvizia na mengineyo.
-BBC