CCM Ikifunga Kampeni za Udiwani Kata ya Bugarama, Shinyanga

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia mamia ya wananchi katika mkutano wa kufunga kampeni za CCM za udiwani Kata ya Bugarama, Kahama mkoani Shinyanga, Oktoba 27. (Picha na Bashir Nkoromo)


Nape akihutubia mkutano wa kampeni a uchaguzi mdogo wa Udiwani Kata ya Bugarama, Kahama mkoani Shinyanga


Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akisalimiana kw furaha na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja walipokutana katika Kata ya Kakola, kabla ya kwenda kwenye mkutano wa kufunga kampeni za udiwani za CCM kata ya Bugarama mkoani humo. (Picha na Bashir Nkoromo)


Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige (kushoto) akimlaki Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alipowasili Kahama mkoani Shinyanga kwa ajili ya kufunga kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Bugarama, mkoani humo. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kahama, Mabala Mlolwa. (Picha na Bashir Nkoromo)


Madiwani wa Kata za Kahama wakiwa na mgombea Udiwani wa CCM, Kata ya Bugarama katika wilaya hiyo Nixon Ikoko wakati wa mkutano wa kufunga kampeni za udiwani katika kata hiyo, uliohutubiwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye. (Picha na Bashir Nkoromo)