Mahafali ya Chuo Kikuu Huria Jijini Dar es Salaam Leo
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa (kushoto) akiwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Ali Juma Shamuhuna (kulia) wakiongoza maandamano ya viongozi anuai na wahadhiri wa chuo hicho, kabla ya kuanza kwa hafla ya Mahafali ya Chuo Kikuu Huria (OUT) cha Tanzania yaliofanyika leo (27/10/2012). Katika Mahafali hayo yaliyofanyika Mkoa wa Pwani, Kibaha, ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda jumla ya wahitimu 2937 walifuzu katika hatua mbalimbali.
Wanafunzi wanaotunukiwa shahada mbalimbali Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) wakiwa katika hafla hiyo na majoho yao leo wakisubiri kukabidhiwa vyeti na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda katika Viwanja vya Makao Makuu ya Kudumu ya chuo hicho yaliopo Kibaha. Jumla ya wahitimu 2937 wametunukiwa shahada mbalimbali.
Hapa tunapata picha ya kumbukumbu..! Baadhi ya wanamahafali wakipiga picha za ukumbusho.
Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wa wahitimu wakinunua zawadi na mapambo kwa wanamahafali wao kama ishara ya kuwapongeza jirani na eneo la mahafali hayo Kibaha.
Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wa wahitimu wakinunua zawadi na mapambo kwa wanamahafali wao kama ishara ya kuwapongeza jirani na eneo la mahafali hayo Kibaha.