Bondia Gottlieb Ndokosho wa Namibia Kutafutiwa Mbabe Wake

Ndoshoko kulia akimsulubu mpinzanai wake

BONDIA kutoka nchini Namibia, Gottlieb Ndokosho ambaye alimsambaratisha Mtanzania, Rajabu Maoja katika raundi ya kwanza ya mpambano wao wa kugombea mkanda wa IBF Afrika uzito wa unyoya, atapanda tena ulingoni jijini Windhoek, Namibia kutetea mkanda huo kati ya mabondia watatu ambao walipendekezwa na IBF kuzichapa nae.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Rais wa IBF Africa Masharikim ya Kati, Ghuba za Uarabu na Uajemi, Onesmo Ngowi, mpambano huo utakaofanyika katika jiji la Windhoek nchini Namibia utatoa upinzani mkali sana kati ya mabondia hao wanaochipukia vyema.

Bondia Helen Joseph ameshapigana mapambano 13 na amepoteza mara mona wakati mpinzani wake Dahianna Santana amepigana mara 37 na kupoteza mara 6.


Hata hivyo taarifa zinasema kati ya majina matatu yaliyopendekezwa na IBF limo jina moja la Mtanzania Fredy Sayuni ambaye anaishi jijini Dar-es-Salaam. Wengine ni Patric Okine kutoka Ghana na David Kiilu kutoka nchini Kenya.

Wakati huo huo; Bara la Afrika litapigania ubingwa wake wa dunia. Mpambano huo utawakutanisha Helen Joseph kutoka nchi ya Nigeria akikutana na bondia Dahianna Santana kutoka Dominican Republic huko Latin America ambaye ndiye bingwa wa dunia wa IBF katika uzito wa unyoya (featherweight) kwa upande wa wanawake.

Mpambano huo utafanyika Decemba 1 katika jiji la San Domingo na litasimamiwa na Rais wa IBF katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati, Ghuba za Uarabu na Uajemi, Mtanzania Onesmo Ngowi. Bondia Helen Joseph ameshapigana mapambano 13 na amepoteza mara mona wakati mpinzani wake Dahianna Santana amepigana mara 37 na kupoteza mara 6.