Na Mwandishi Wetu
KAMISHENI ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC) imetoa kibali kwa bondia Rashid Ally kupigana na Bondia Wilson Masamba wa Malawi katika Motel Paradise jijini Blantyre nchini Malawi 28th Oktoba, 2012.
Mpambano huo wa round nane katika uzito wa unjoya (feather weight) utakuwa sio wa ubingwa na utakuwa mpambano wa 50 kwa bondia Rashid Ally wakati kwa bondia Wilson Masamba utakuwa mpambano wa 24. TPBC inamshauri bondia Rashid Ally ajiandae vizuri ili aweze kupeperusga bendera ya Tanzania vyema nchini Malawi na kuendeleza ushirikiano na urafiki wa nchi hizi mbili.
Aidha, TPBC inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu mikataba mbalimbali ya ngumi inayotiwa sahihi na mabondia wa kitanzania. Mikataba ya ngumi duniani kote hairuhusu kutolewa kwa pesa za maandalizi au awali (advance payment) kwa mabondia wanaopambana.
Mikataba ya ngumi husainiwa kwa bondia aliyesaini kupewa pesa yake yote baada ya kushuka kwenye ulingo. Hizi nisheria za kimataifa na mabondia wanaoendekeza tabia ya kupewa pesa za awali (advance payment) wanapotosha umma na kutia doa tasnia ya ngumi za kulipwa Tanzania.
Imetolewa na: Uongozi, Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC)