Dk. Shein Awaapisha Viongozi Wapya Aliowateuwa Katika Mabadiliko

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akimuapisha, Mtumwa Kheir Mbarak kuwa Naibu Waziri Kilimo na Maliasili, katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo. (Picha na Ramadhan Othman, Ikulu)


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akimuapisha, Saidi Mohamed Said kuwa Naibu Waziri Mifugo na Uvuvi, katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo. (Picha na Ramadhan Othman, Ikulu)


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein akimuapisha, Shawana Bukheti Hassan kuwa Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo. (Picha na Ramadhan Othman, Ikulu)

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein leo amewaapisha wajumbe wapya wa Baraza la Mapinduzi ya Zanzibar (BMZ) aliowateuwa katika mabadiliko aliyoyafanya juzi. Katika hafla hiyo iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar, Dk. Shein amewaapisha jumla ya wajumbe watatu wa baraza hilo pamoja na manaibu katibu wakuu kutoka katika wizara nne tofauti za Serikali yake.

Walioapishwa ni pamoja na Shawana Bukheti Hassan ambaye anakuwa Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi, Saidi Mohamed Said anayekuwa Naibu Waziri Mifugo na Uvuvi, na Mtumwa Kheir Mbarak ambaye ameteuliwa kuwa Naibu
Waziri Kilimo na Maliasili.

Rais Dk. Mohamed Shein pia amewaapisha Tahir M. Abdulla kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano, Mustafa Aboud Jumbe kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Makaazi, Maji na Nishati, Julius Nalimy Maziku kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Idara Maalum za SMZ pamoja na Juma Ameir Hafidh anayekuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais (Fedha Uchumi na Mipango ya Maendeleo).

Hafla hiyo pia imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa vyama na Serikali ya Zanzibar.