Silafrica Yakabidhi Msaada wa Tanki la Maji Kituo cha Polisi Buguruni

Meneja Mkuu wa Kampuni ya Vifaa vya Plastiki-Silafrica Limited (SIM TANK), Alpesh Patel (wa pili kushoto) akisalimiana na Msaidizi Mkuu wa Kituo cha Polisi Buguruni, Batseba S. Kassanga muda mfupi baada ya kampuni ya Silafrica kukabidhi msaada wa tenki la maji lenye uwezo wa kubeba maji lita 2000 litakalotumiwa na kituo hicho. Katikati ni Meneja wa moja ya gala la Silafrica, Salim Mohamed wengine ni maofisa wa Kituo cha Polisi Buguruni.

Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya vifaa vya plastiki Silafrica Limited (SIM TANK) jana ilikabidhi tanki lenye uwezo wa kuchukua lita za ujazo 2000 za maji kwa ajili ya kuhifadhia maji safi katika kituo cha poilisi cha buguruni jiji Dar es Salaam katika hafla fupi iliyofanyika kituoni hapo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla hiyo, Meneja Mkuu wa kampuni ya Silafrika Limited, Alpesh Patel alisema kampuni yake inatambua umuhimu wa jamii inayoizunguka na kwamba wanayo jukumu kubwa la kusaidia jamii hiyo hasa katika maswala ya kijamii kama sehemu mojawapo ya kurudisha shukrani zao kwa wateja wao na watanzania kwa ujumla.

“Silafrica limited tunajaribu kujisogeza zaidi karibu na jamii inayotuzunguka na kuweza kushirikiana kwapamoja kutatua mataizo mbalimbali yanayohusu jamii ya watanzania,” alisema Patel na kuongeza kuwa sekta binafsi inayo jukumu kubwa la kutumia kiasi kidogo cha mapato yake katika kusaidia jamii kwani kwa kufanya hivyo maendeleo ya jamii inayoizunguka yataonekana yakipiga hatua.
Silafrica imefikia hatua hiyo baada ya tanki lililokuwa kituoni hapo kuchakaa vibaya na kutoboka hali ambayo imepelekea kituo hicho kupata uhaba wa maji safi kwaajili ya matumizi ya binadamu kituoni hapo ambapo kampuni hiyo imejitolea fundi wa kufanya matengenezo ya mabomba kituoni hapo.
Kwa upande wake mkuu wa kituo cha polisi cha buguruni Assistant Superintendent Batseba S. Kassanga, ameishukuru sana kampuni ya Silafrica limited kwa kuona umuhimu wa maji safi kituoni hapo na kuamua kujitolea kusaidia swala la maji.

“Kila mtu anatambua fika kuwa maji safi ni uhai katika maisha ya binadamu yeyote duniani, napenda kutoa shukrani zangu za dhati kabisa kwa kampuni ya Silafrica limited kwakutuchagua kuwa sehemu yao ya kusaidia katika maswala ya kijamii, kwa niaba ya jeshi la polisi kituo cha buguruni napenda kushukuru sana,” alisema Kassanga huku akiwataka makampuni mengine yajitokeze kuiga mfano wa kampuni ya Silafrica.

Kampuni ya Silafrica limited ni kampuni inayotengeza bidhaa ya plastiki ikiwepo matenki ya kuhifadhia maji aina ya SIM TANK ambayo imekuwa ikfanya vizuri sana kwa ubora wake.