Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji mke wa aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow, wakati alipofika nyumbani kwa marehemu Ukonga jijini Dar es Salaam, leo Oktoba 16, kushiriki katika shughu za msiba huo na kutoa heshima za mwisho wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa marehemu huyo aliyeuawa hivi karibuni jijini Mwanza. Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akitia saini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow, wakati alipofika nyumbani kwa marehemu Ukonga jijini Dar es Salaam, leo Oktoba 16, kushiriki katika shughu za msiba huo na kutoa heshima za mwisho wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa marehemu huyo aliyeuawa hivi karibuni jijini Mwanza. Picha na OMR
*Mwili wake Wasafirishwa Kwenda Kilimanjaro Kwa Mazishi
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal leo ameongoza viongozi mbalimbali wa chama na Serikali, maofisa wa jeshi na baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kutoa salamu za mwisho kwa mwili wa malehemu Kamanda Liberatus Barlow nyumbani kwake Ukonga.
Marehemu Barlow aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, aliuawa juzi usiku kwa kupigwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi maeneo ya Kitangiri jijini Mwanza mara baada ya kuagwa amesafirishwa kuelekea mkoani Kilimanjaro kwa mazishi yanayotarajia kufanyika kesho kijijini kwao.