King Class Mawe Afuliwa Kumkabili Bondia Segu

Kocha wa mchezo wa Ngumi Habibu Kinyogoli (kulia) akimfua bondia Ibrahimu Class ‘King Class Mawe’ kwa ajili ya mpambano wake na Jonas Segu Oktober 14 jijini Dar es Salaam.

BONDIA Ibrahimu Class ‘King Class Mawe’ yupo katika mazoezi makali kwa ajili ya mpambano wake na bondia Jonas Segu litakalofanyika Oktoba 14, 2012 ikiwa ni siku ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julias Kambarage Nyerere katika Ukumbi wa Friends Corner, Manzese jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi Rajabu Mhamila ‘Super D’ ‘alisema kuwa wana muandaa ‘King Class Mawe’ kwa ajili ya mpambano wake huo. “Tunamuandaa vizuri kwa pambano hilo ili aje kuwa bondia bora wa masumbwi hapa nchini, unajua kuna staili nyingi za mazoezi ambazo anapewa bondia kumkabili mpinzani wake,” alisema.

Super D aliongeza kuwa mazoezi anayofanyishwa ‘King Class Mawe’ kwa sasa akuna mtu anaweza kumfikia kwa kuwa kashavuka viwango bondia huyo anaecheza katika uzito wa Kg 60 amekuwa tishio kwa mabondia wezake baada ya mchezo wake wa mwisho kumdunda SakoMwaisege kwa K,O raundi ya tatu katika ukumbi wa Diamond Jubilee Hall, Dar-es-Salaam.

Na ataendeleza kupiga wapinzani wake kwa K,O katika raundi za mwanzo bila kuwachosha majaji pamoja na refarii wake. Aliongeza kwa Super D kuwa wanamfanyisha mazoezi ya kupiga kwa K,O ili aweze kuendeleza rekodi aliyonayo kwa sasa kwani mapambano yako yote matatu aliyocheza kapiga wapinzani wake wa K,O.