Yanga na Simba Zatoka Sare ya 1-1

Baadhi ya wachezaji wa Simba wakishangilia goli lao la mapema lililofungwa dakika 4 ya mchezo. Picha kwa hisani ya FullShangwe Blog)

TIMU za Yanga na Simba zote za jijini Dar es Salaam leo zimeshindwa kuoneshana ubabe baada ya kujikuta zinatoka sare ya goli moja kwa moja. Simba ndiyo waliokuwa wa kwanza baada ya kuanza kuifunga Yanga katika dakika ya nne tu ya mchezo huo ambao ulikuwa na vuta nikuvute nyingi.

Goli la Simba lilidumu hadi timu zilipokwenda mapumziko. Yanga walifanikiwa kupata goli lao kwa njia ya penati baada ya mmoja wa wachezaji wa Simba kujikuta akiunawa mpira kwenye eneo la hatari, ambapo mwamuzi aliamuru ipigwe penati ambapo yanga walipata goli la kusawazisha. Hadi dakika ya 90 mwamuzi wa pambano hilo akipuliza kipenga cha mwisho timu zote zilitoka 1-1. Kwa matokeo hayo Simba anaendelea kuongoza Ligi Kuu ya Tanzania Bara.