Mafunzo ya Taiching Kumfuu Kutolewa

Masta Jumanne

Na Mwandishi Wetu

MSANII Jumanne Wilsoni ‘Masta Jumanne’ amewashauri vijana kujiunga na mazoezi yanayotolewa katika Ukumbi wa Ilala Sheli- CCM, ambapo anafundisha mchezo wa ‘Taiching Kumfuu’ mafunzo yanayowasaidia vijana kujilinda wenyewe na kuimarisha afya zao.

Amewataka vijana kujitokeza kufanya mazoezi katika staili mpya mbalimbali alizokuja nazo toka China hivi karibuni za ‘Taichi Kung-fu’ kwa ajili ya kufanikisha kujilinda wakati wowote na watu wabaya. Masta Jumanne aliyejifunzia michezo hiyo nchini China na akiwa ni wa kwanza kuingiza staili hiyo nchini kwa ajili ya kukuza vipaji vya mchezo wa Taichi Kung-fu, alisema mafunzo kama hayo pia hutolewa Ilala CCM Mchikichini.

Alisema alianza kufundisha mwaka 2003 katika Majeshi ya Tanzania na sasa anawafundisha raia mbalimbali kwa ajili ya kujilinda. Masta Jumanne ambaye anatamba na filamu ya mapigano ijulikanayo kwa jina la Malipo ni Duniani ‘ alisema filamu hiyo ametoa ili kuonesha dunia jinsi ilivyo na malipo yake hapa hapa.

Anasema sasa yupo mbioni kutoa filamu ya nipo trayari kufa inayotarajia kutoka mwishoni mwa mwezi uhu iliowashilikisha raia wa kichina ambayo ipo katika matasifa mawili ya Tanzania na China. Mpaka sasa ameshawafundisha vijana wapatao 60 ambao wamepitia mafunzo kutoka kweke.

Masta Jumanne kabla ya kwenda kujiendeleza zaidi na mafunzo ya mchezo huo katikla nchi mbalimbali alikuwa ajifunza nchini Zambia kabla ajaenda china kukamilisha mafunzo yake ya ufundishaji. Ametoa wito kwa watu mbalimbali kujitokeza katika mafunzo yake kwa kuwa wengi aliowafundisha wamepata mafanikio mbalimbali kupitia kwake ikiwemo kupata ajira katika makampuni mbalimbali ya ulizi na usimamizi wa shunghuli mbali mbali za kitaifa. Mawasiliano 0713938461.