Mtoto mwenye umri wa miaka nne, Nyambuli Mganga akiwa na kikundi cha sanaa na utamaduni kijulikanacho kwa jina la Utandawazi Theatre Group Matwigha Chalo kutoka Nansole Ukerewe akionyesha umahiri wake wa kucheza ngoma ya Ukerewe inayojulikana kwa jina la Obusimbula kwa wahitimu katika sherehe za mahafali ya 23 ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSUBa). Sherehe hizo ziliambatana na kilele cha maonesho ya 31 ya Tamasha na Sanaa na Utamaduni liliyofanyika katika ukumbi wa taasisi hiyo iliyopo Bagamoyo, Mkoa wa Pwani, Nyambuli ambaye anarithi utamaduni huo kutoka kwa mama yake, Wiliherimina Kebela, ambaye yuko katika kikundi hicho.
Mtoto Nyambuli Mganga akiendeleza burudani hiyo meza kuu
Baadhi ya wahitimu wa Stashahada ya Juu ya Sanaa na Utamaduni wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasm Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSuBa), Profesa Elias Jengo(kushoto) ambaye ni Mhadhili wa taaluma hiyo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)i, aliyeko katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Vijana, Profesa Hermas Mwansoko na kulia kwake ni Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo, Juma Bakari. Wengine ni baadhi ya wakufunzi.