Mahoja Awatio Hofu Namibia

MTANZANIA Rajabu Maoja amelitingisha jiji la Windhoek, nchini Namibia alipoingia katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Hosea Kutako. Maoja aliingia kwa mbemwe za aina yake baada ya kukataa kukumbatiana na wenyeji wake ambao walikuwa na shauku ya kumkumbatia.

Akiwa na sura ya kujiamini huku akitembea kibabe Mtanzania Maoja alionyesha nia ya kuuchukua mkanda wa ubingwa wa IBF katika bara la Afrika wakati atakapoumana na bingwa wa Namibia Gottlieb Ndokosho siku ya Jumamosi tarehe 29, Septemba.

Mpambano huo ulipewa jina la Vita Vya Jangwa wa Kalahari (The Battle for the Kalahari Desert) na waandaaji wake ambao ni kampuni ya Kinda Boxing Promotions inayoongozwa na Simon Nangolo limeleta shamrashamra za aina ya pekee katika ukanda huu wa Kusini mwa jangwa la Sahara.

Mpambano huo ni moja ya mapambano ambayo yapo kwenye programu ya Utalii wa Michezo ya IBF (IBF Sports Tourism) ambayo inasimamiwa na Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF) na kuratibiwa na Rais wa IBF katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi, Mtanzania Onesmo Alfred McBride Ngowi.

Nao mabondia kutoka Zimbabwe na Afrika ya Kusini ambao watacheza mapambano ya awali wameshafika na tayari shamrashamra za mpambano huo zimeshika kasi kwa wadau na wapenzi wa ngumi wa nchi ya Namibia na nchi jirani kama Botswana, Afrika ya Kusini, Lesotho na Swaziland.

Hata hivyo hii ni mara ya kwanza kwa ushindani mkubwa namna hiyo kuwahi kutokea katika jiji la Windhoek Namibia, Mpizania wa Maoja Gottlieb Ndokosho ameingai mitini na hajaonekana tangu kuingia kwa Mahoja Jijini hapa.

Kesho ni kesho na Watanzania wamuombee mwakilishi wao ili aweze kuipeperusha vizuri bendera ya Tanzania!

Mungu mbariki Rajabu Jumanne Maoja, Mungu ibariki nchi nzuri ya Tanzania.