Ijue bendi ya ‘FFU’ ya nchini Ujerumani

Mmoja wa wasanii nguli wa kundi la 'FFU'

“The Golden Voice of East Africa”

 BENDI maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band, ni bendi ya kwanza ya kiafrika iliyojiwekea nafasi ya pekee katika nyoyo za washabiki uko ughaibuni. Bendi hiyo ambayo inatajwa kuwa ndio bendi ya kwanza ya kiafrika kutumia muziki wake kutoka uswahilini kama daraja la kuwafikia washabiki wake katika kona zote duniani, pia imetajwa na vianzo vya habari vya kimataifa  kuwa mdundo wa mziki wake umekuwa ni urimbo unao wanasa na kuwatia kiwewe washabiki, popote pale duniani.

 Bendi ya Ngoma Africa band aka FFU yenye maskani yake nchini Ujerumani ilianzishwa mwaka 1993 na mwanzilishi kwake mwanamziki Ebrahim Makunja almaarufu pia kwa majina kama Ras Makunja kamanda wa FFU, ambaye  pia ndiye mtunzi, mwimbaji na kiongozi wa bendi hiyo, bendi hiyo ina utajili wa wanamziki wenye vipaji baadhi yao wakiwemo mpiga solo gitaa Christian Bakotessa aka Chris-B aka “Mshenzi” wa solo gitaa ambae pia yupo katika safu ya uimbaji, Wengine ni Maxime Buanda aka “Kapteni wa mapenzi” na Saidi Jazbo Vuai wapiga bass gitaa, Willy Mbiya(Drum), wapo akina dada Severn Okomo na Bedi Bella, bendi hiyo maarufu ina wanamziki takriban wanane, bendi hiyo pia imezungukwa na wataalamu akiwemo Bw. Mfundo Peter Mufundo, ambaye ni mtayarishaji msaidizi wa mziki

Ngoma Africa band ni bendi iliyo pachikwa majina mengi ya utani au usanii kama vile FFU, Mzimu wa Muziki, Wazee wa kukaanga mbuyu, majina ambayo bendi hiyo haiwezi kuyakwepa !  Jina lingine ambalo lilikua gumu kwao kulikubali ni “Watoto wa Mbwa” bendi hiyo ilibandikwa jina hilo na baadhi ya wadau wa mziki, kuwa nyimbo zao ni sawa vitisho vya mbwa wanao bwaka katika kila sekta na kugusa nyoyo za walio wengi !

 Ngoma Africa band imefanikiwa kufyatua CD nyingi ambazo nyimbo zilizomo katika santuri hizo zinatawala anga za redio za kimataifa..na kulitangaza kwa kasi kubwa jina la Tanzania kanji ya muziki , baadhi ya nyimbo zao ni pamoja “Rushwa ni adui wa haki” , Album “Mama Kimwaga”, Single CD “Apache wacha Pombe” , CD “Jakaya Kikwete 2010” ambazo zote ni Utunzi wake kiongozi wa bendi hiyo kamanda Ras Makunja wa FFU,mjeshi wa ambaye kufanya nae kazi inataka uwe na tabia za ki FFU, yaani uwe tayari tayari wakati wowote kwenda kutumbuiza hata ikiwa katika nchi za vita ! Na mdundo anautaka yeye lazima uwe na mwendo wa kasi na magitaa Lazima yalie milio ya kushambulia mashabiki katika ulingo wa dansi, mdundo ambao umepewa jina “Extra Ordinary” Bongo Dance, mdundo ambao umefanikiwa kuwateka na kuwanasa na kuwatia kiwewe watu wengi katika kila kona duniani, Wasikilize at www.reverbnation.com/ngomaafricaband au

Pia wana website yao www.ngoma-africa.com ambayo mpenzi Au mshabiki anaweza ku log in na kujumuika nao kama mwanachama wa bendi hiyo.

Ngoma Africa band inaonekana kuwa na mfumo tofauti sana ! Kuwa

Washabiki wanasauti kubwa ya kuweza kulazimisha maonyesho kuliko

uongozi wa bendi !? Mashabiki mara nyingi wamekua tishio hadi kwa

maporomota na waandaaji wa maonyesho makubwa ya mziki…kama

Bendi ya Ngoma Africa haikualikwa au kupangwa katika ratiba ya onyesho

Fulani basi wapo tayari kususia onyesho hilo…au pengine wakalivunja !

Tena washabiki  hao wa umri wa lika na mataifa mbali mbali hawaoni wala

hawasikii kitu kingine chochote mbele Bongo dansi la Ngoma Africa band

aka FFU,ukipenda waite “Watoto wa Mbwa” majina yote size yao !

maporomota au waandaaji wa maonyesho mengi ya mziki huko ughaibuni

wanalazimika kuandaa ulinzi wa kutosha mara tu wanapoalika bendi hiyo kushiriki katika maonesho yao..hapa ndipo vianzo vingi vya habari vya ndani

na nje ya nchi vinapofika katangaza kuwa FFU wa Ngoma Africa band “jino kwa jino”

au “Jicho kwa Jicho”

Ras makunja aka kamanda wa FFU na mzimu wake Ngoma Africa band,wamefanikiwa kwa

kiasi kikubwa kuutangaza mziki wa bongo, na kuliweka jina la Tanzania kimziki katika nafasi ya

juu kimataifa ,hakuna asiejua kuwa kazi ya usanii wa mziki inahitaji kudata akili kiana yake hili

kuhakikisha kile unachokipigania “Mziki” kunafika kilele cha kimataifa…

vichaa wetu hawa wa mziki Ngoma Africa band aka FFU aau ” Watoto wa Mbwa” wameidatia

akili kazi yao ya mziki, leo hii wana ngome yao hii www.ngoma-africa.com