‘FFU’ wa Ngoma Africa Band Watimua Vumbi Afrika-Messe

FFU walipotua Bremen

KIKOSI kazi cha Ngoma Africa Band iliyozoeleka kwa tendo la kuwapagawisha washabiki wa muziki ughaibuni, Septemba 15, 2012 kimefanya kweli katika maonesho makubwa ya biashara ya Afrika-Messe, mjini Bremen, Ujerumani.
Bendi hiyo maarufu ilipanda jukwaani na kufanikiwa kuziteka nyoyo za washabiki kwa mara nyingine tena kwa kuwadatisha akili na muziki wenye raha kamili. CD za bendi hiyo zimekamata nafasi ya juu katika vituo mbali mbali vya Redio ndani na nje ya Ughaibuni, baadhi ya vituo vya radio zikiwamo
Redio maarufu nchi Ujeruamani Radio Funkhaus Europa na Radio Mult-Kult ndizo zinarusha kwa fujo nyimbo za Ngoma Africa band, inayoongozwa na kamanda Ras Makunja wa FFU.

Unaweza kuwasikiliza pia katika kambi yao at http://www.ngoma-africa.com au www.ngoma-africa.com