Rais Mpya wa Somalia Atawazwa

Rais mpya wa Somalia, Hassan Sheikh

Rais mpya wa Somalia atawazwa

RAIS mpya wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud, ametawazwa rasmi kwenye sherehe iliyofanywa mjini Mogadishu. Kiongozi huyo mpya, ambaye alinusurika na jaribio la kumuuwa Jumatano, alisema mambo muhimu kwake ni usalama na mapatano.

Viongozi kadha wa kanda walihudhuria sherehe hiyo pamoja na waziri mkuu mpya wa Ethiopia, Hailemariam Desalegn, na rais wa Djibouti, Ismail Omar Guelleh. -BBC