‘FFU’ Watembeza Gwaride la Kufa Mtu Ughaibuni

Klimahaus Bremerhaven mjengo wa ajabu ambapo FFU wamefanya onesho lao


*Ni katika Jumba la ajabu palikua hapatoshi


KIKOSI
kazi cha wasanii wa Ngoma Africa Band a.k.a FFU, yenye maskani yake nchini Ujerumani Septemba 12, 2012 ilijikuta ikivaana jino kwa jino na washabiki wakongwe ndani ya juma la ajabu la “Klimahaus” Arena mjini Bremerhaven, Ujerumani.

Baada ya mdundo wa ngoma africa band kupenya katika nyoyo za washabiki wa mataifa mbali mbali
walifurika katika onesho hilo wengi wao wakiwa wenyeji wa ulaya. Uwanja wa dansi ulionekana
mdogo na kukawa na patashika la nguo kuchanika.

Washabiki waliodata akili walijikuta wakiperekana samba samba na muziki wa ngoma africa band,
kiasi cha kuwafanya walinzi wa usalama kufanya kazi ya ziada kuhakikisha kila kitu kipo salama.

Ngoma Africa band aka ffu au maarufu kwa majina mengi ya utani kama vile “Watoto wa Mbwa”
“wazee wa bongo tambarare” kutoka katika kabila la “Wagagagigikoko” waliogunduliwa katika
Maadiko ya kitabu cha Buri Cheka watatumbuiza tena siku ya Jumamosi 15.09.2012 katika
Maonyesho ya AFRIKA-MESSE mijini Bremen, Ujerumani.

Usikose kuwasikiliza at www.ngoma-africa.com