Mkuu wa Itifaki wa Miss Tanzania Albert Makoye akifungua mashindano ya Redd’s Miss Kinondoni Talent, pembeni yake ni Ssebo ambaye ni mmoja kati ya mwanabodi wa Redd’s Miss Kinondoni 2012 na alikuwa ni mshereheshaji katika shindano hilo lililofanyika katika hoteli ya JB Belmonte, iliyopo jengo la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Mashindano hayo yalidhaminiwa na Perfect Lady Classic Saloon iliyopo Kinondoni jijini Dar na wametoa zawadi kwa washindi watatu waliopatikana kwa kupewa huduma kwa kipindi cha mwaka mzima ndani ya Saloon yao. Shindano rasmi la kumsaka Redd’s Miss Kinondoni linatarajiwa kufanyika Ijumaa tarehe Septemba 14, 2012 katika Ukumbi wa Cassa Complex uliopo Mikocheni, Dar.
Mshiriki namba 6, Irene akionyesha manjonjo yake katika kucheza.
Mshiriki namba 3, Nahma Saidi yeye aliambua kuonyesha mambo ya Pwani.
Mshiriki namba 1, akionyesha umahili wake wa kukata uno.
Mshiriki namba 4, Diana Hussein akionyesha jinsi ya kubuni vazi.
Brigitter Alfred mshiriki namba 9 alionyesha umahili wake katika nyimbo za kihindi.
Majaji wa shindano la Redd’s Miss Kinondoni Talent Man Maji (kulia) na mwanadada wakifuatilia kwa makini.
Mshiriki namba 10, Kudra Lupatu akionyesha kipaji chake cha kubuni mavazi kwa staili ya kumvalisha mshiriki mwenzake.
Kudra Lupati katika pozi mara baada ya kumaliza kutambulisha vazi lake.
Mshiriki wa Redd’s Miss Kinondoni akichora mlima Kilimanjaro.
Ssebo ambaye ni mmoja kati ya mwanabodi wa Redd’s Miss Kinondoni 2012 na alikuwa ni mshereheshaji katika shindano hilo la Talent akimkaribisha Mratibu wa Redd’s Miss Kinondoni 2012, Vivien Sirikwa (kulia) kuongea machache.
Mkurugenzi wa Perfect Lady Classic Saloon, Ester Kiama ambao ndiyo waliokuwa wamedhamini Redd’s Miss Kinondoni Talent akitangaza zawadi alizowapatia warembo walioshinda.
Wakiwa katika nyuso za furaha ni warembo walioshinda katika Kinyang’anyiro cha Redd’s Miss Kinondoni Talent kutoka kulia ni Judith Sangu, Brigitter Alfred na Diana Hussein. Warembo hao wamepatiwa zawadi ya kupewa huduma Perfect Lady Saloon kwa kila mmoja kipindi cha Mwaka mzima.
Warembo wakiserebuka mara baada ya shindano hilo kuishi.
…Hapa ni mwendo wa Kwaito… Katika Redd’s Miss Kinondoni 2012 .