Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa (katikati), Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Makongoro Mahanga (kulia), Mkurugenzi wa Mahusiano ya Serikali wa Kampuni ya African Barrick Gold, Emmanuel Ole Naiko (pili kushoto) na Meneja Mawasiliano wa African Barrick Gold, Nector Pendaeli (kushoto) wakiwaangalia wanafunzi wa Shule ya Msingi Minazi Mirefu, iliyopo eneo la Kipawa Banana, Jijini Dar es Salaam leo waliokuwa wameketi kwenye sehemu ya Madawati 500 yaliyokabidhiwa na Kampuni ya African Barrick kwa shule hiyo. Hii ni sehemu ya Jitihada zinazofanywa na Diwani wa Kata ya Kipawa, Bi. Boma Kaluwa kwenye kuinua maendeleo ya kata yake.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akizungumza mara baada ya kukabidhi madawati hayo kwa Shule ya Msingi Minazi Mirefu iliyopo eneo la Kipawa Banana,Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira na Mbunge wa Jimbo la Segerea, Makongoro Mahanga akizungumza machache na kutambulisha baadhi ya wageni waliohudhulia katika hafla hiyo fupi ya kukabidhi madawati 500 kwa shule ya Msingi Minazi Mirefu, iliyopo eneo la Kipawa Banana, Jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa akimkabidhi cheti Mkurugenzi wa Mahusiano ya Serikari wa Kampuni ya African Barrick Gold, Emmanuel Ole – Naiko wakati wa hafla ya kukabidhi madawati 500 katika Shule ya Msingi Minazi Mirefu iliyopo eneo la Kipawa Banana,Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Rotary tawi la Mzizima, Mustafa Kundrati akizungumza katika hafla hiyo. Rotary Mzizima nao wamekuwa mstari wa mbele katika maendeleo ya kata hiyo kwa kujenga visima vingi vya maji katika shule kadhaa zilizopo katika kata ya Kipawa.
Walimu na Baadi ya viongozi wakiburudika kwa muziki wakati wakimkaribisha mgeni rasmi, ambaye ni Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa (hayupo pichani).
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa akisalimia na baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Msingi Minazi Mirefu, iliyopo eneo la Kipawa Banana, Jijini Dar es Salaam wakiompokea kwa shangwe na bashasha tele.