Taarifa kuhusu Kongamano la kujadili haki za binadamu Tanzania, uhuru wa kupata habari na tishio la usalama kwa watetezi wa haki za bindamu

Taarifa kuhusu Kongamano la kujadili haki za binadamu Tanzania, uhuru wa kupata habari na tishio la usalama kwa watetezi wa haki za bindamu litakalofanyika katika viwanja vya Mtandao wa Jinsia (TGNP) Mabibo Dar es Salaam siku ya Jumatano

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI YAHUSU KONGAMANO LA WADAU WA SEKTA YA HABARI, WATETEZI NA WANAHARAKATI WA HAKI ZA BINADAMU TANZANIA

Ndugu wanahabari,
Kufuatia hali tete inayowakabili watetezi wa haki nchini Tanzania, mtandao wa Watetezi wa Haki za Bidamu Tanzania (THRD) umeamua kuwakutanisha wadau muhimu katika utetezi wa haki za binadamu, asasi mbali mbali za kiraia na viongozi wa dini ilikujadili namna ya kuzuia wimbi la vitendo vya kikatili na ugandamizaji wa haki za binadamu kwa ujumla.
Ni kwa kuzingatia muktadha huu Mtandao wa Watetezi umeandaa kongamano la siku moja litakalojadili hali ya haki za binadamu nchini Tanzania, uhuru wa kupata habari na tishio la usalama kwa watetezi wa haki za bindamu litakalofanyika katika viwanja vya Mtandao wa Jinsia (TGNP) Mabibo Dar es Salaam siku ya Jumatano tarehe 12 Agosti, 2012 kuanzia saa 4:00 mpaka saa 7:00 mchana.
Kongamano hilo linakuja wakati familia nyingi wakiwamo akina mama na watoto wakiwa hawajui maisha yao ya baadaye yatakuwaje baada ya kufiwa na wapendwa wao wakiwamo wazazi ambao bado walikuwa wanahitajika katika malezi ya familia zao.
Matukio ya hivi karibuni kabisa yamewahusisha mashabiki na wapenzi wa chama kikuu cha upinzani kwa sasa Chama cha Demokrasia na Maendeleo kwa upande mmoja na Jeshi la Polisi kwa upande mwingine.
Ipo hatari ya wazazi kuanza kuwazuia watoto wao wasihudhurie kabisa mikutano ya chama hicho, lakini kwa upande mwingine ipo hatari ya wanachi kupoteza imani na Jeshi la Polisi ambalo kimsingi linawajibu mkubwa wa kulinda usalama wa raia na mali zao. Na zaidi ya hayo iwapo watu wataanza kuamini kwamba jeshi hilo linatumika kisiasa basi ipo hatari ya kuibuka kwa vyombo vingine vitakavyojivisha jukumu la kuwalinda Watanzania na mali zao.
Kwa lengo jema la kurudisha imani ya wananchi kwa jeshi lao, kwa wanaharakati za binadamu kuendelea kufanya kazi bila vitisho na kwa waandishi wa habari kuhakikishiwa usalama wao kazini, wadau wote wakiwa ni wanazuoni katika fani za habari, sheria, haki za bainadamu na walaji wote wa kazi za habari wanaombwa kuhudhuria na kutoa michango ya mawazo yao.
Historia inaonyesha kwamba kumekuwapo na mauaji yanayohusiha wanasiasa kama ifuatvyo; Arusha katika sakata la kumpinga meya wa mji huo ambapo watu watatu waliuawa, Igunga, Singida, Morogoro na tukio la hivi karibuni kabisa la mauaji ya kinyama ya mwandishi wa habari wa televisheni ya Channel Ten, Daudi Mwangosi.
Matukio mengine ni lile la kutekwa kuteswa na kIsha kutelekezwa porini kwa Daktari Stephen Ulimboka aliyekuwa mstari wa mbele katika kutetea haki za wagonjwa na madaktari, na pia lipo tukio la kufungiwa kwa gazeti huru la uchunguzi la Mwanahalisi.
Wote mnakaribishwa.

Imetolewa na sekretariati ya THRD,

ELIAS MHEGERA- 0754-826272
KAIMU MRATIBU.

WASEMAJI
1. MISA-TAN
2. TGNP
3. MCT
4. TEF
5. MOAT
6. LHRC
7. UTPC
8. Jenerali Ulimwengu (bado anatafutwa kwa hilo haja-confirm)
9. Prof Issa Shivji (bado anatafutwa haja-confirm)