Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa akionyeshwa picha ya mfano wa Kanisa la Moravian Ushirika wa Mbezi Beach jijini Dar es Salaam na Askofu Mkuu wa Kanisa hilo Jimbo la Kusini, Askofu Lusekelo Mwakafwila kabla ya kuanza kwa Harambee ya Kuchangia ujenzi wa Kanisa hilo.Katika harambee hilo iliyoongozwa na Lowassa, jumla ya sh. Mil 70 zimechangishwa.
Mwanadada aleandaliwa kwa kusoma lisala ya kumkaribisha mgeni Rasmi katika kuendesha harambee hiyo, Bi. Leah Mwainyekule akisoma lisala hilo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa akipena mkono na Mkuu wa Mstaafu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Robert Mboma baada ya kuchangia katika Harambee ya Ujenzi wa kanisa la Moravian Ushirika wa Mbezi Beach, Jijini Dar es Salaam,uliofanyika, jumla ya sh. Mil 70 zimechangishwa katika Harambee hiyo.
Meneja wa Kilaji cha Kilimanjaro kutoka TBL,George Kavishe akipena mkono na Askofu Mkuu wa Kanisa la Moravian Jimbo la Kusini, Askofu Lusekelo Mwakafwila mara baada kuchangia katika harambee ya ujenzi wa Kanisa la Moravian Ushirika wa Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.
Kina Mama pia walikuwa Mstari wa Mbele kuhakikisha ujenzi wa Nyumba hiyo ya Mungu unafanyika kwa nguvu zote.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa akipokea Zawadi maalum kutoka kwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Moravian Jimbo la Kusini, Askofu Lusekelo Mwakafwila mara baada ya kuongoza harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya Ujenzi wa Kanisa la Moravian Ushirika wa Mbezi Beach, Jijini Dar es Salaam jana.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Moravian Jimbo la Kusini,Askofu Lusekelo Mwakafwila akitoa neno baada ya kumalizika kwa harambee hiyo.
Kwaya ikiendelea.
Hili ndilo Kanisa linalotakiwa kumalizika ujenzi wake ambalo harambee yake imefanyika leo na kuongozwa na Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa.