Waziri Kenya akutwa na gari la wizi

Waziri wa Serikali za Mitaa nchini Kenya, Fred Gumo

WAZIRI mmoja wa Kenya amekanusha kuwa anahusika na wizi wa gari moja la wizi ambalo amekutwa nalo. Waziri hiyo ambaye ni wa Serikali za Mitaa nchini Kenya, Fred Gumo, alisema gari lake alikuwa amempa mfanyabiashara mmoja wa Mombasa na badala yake akakabidhiwa gari hilo ambalo ni la wizi bila kujua, ambalo lilikuwa limeibwa kutoka kwa rais wa zamani, Daniel Arap Moi, miaka mine iliyopita.

Bwana Gumo amesisitiza kwamba hakujua kuwa gari hilo lilikuwa la kuibiwa. Hata hivyo alisema hakulitumia sana gari hilo kwa sababu hakupata nyaraka zote za gari hilo.

-BBC