Shibuda asema CCM inauchakavu wa fikra

Na Mwandishi Wetu, Thehabari, Maswa 

MBUNGE wa Jimbo la Maswa Magharibi (CHADEMA), John Shibuda amesema CCM ina uchakavu wa fikra na anguko la vitendo linalowatafuna viongozi wake hivyo kushindwa kutambua hisia za wananchi.

Mbunge Shibuda akizungumza bungeni.

Kwamba viongozi hao wamesahau na kuzitupa siasa za Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere kwa kuwa na sera ya kutesa kwa zamu hali inayowanyima haki wananchi ya kufaidi matunda na rasilimali za nchi yao.

Shibuda alitoa kauli hiyo Wilayani Maswa wakati akizungumza na wananchi na wazee wa Jimbo la Maswa Magharibi kuhusiana na changamoto zinazoikabili jamii ya Watanzania.

Alisema viongozi wa CCM wameshindwa kuzibua masikio na kutambua hisia za Watanzania wanahitaji nini ili kuwaletea maendeleo badala yake wanajinadi kujivua gamba kumbe ni funika kombe mwanaharamu apite.

“CCM inauchakavu wa fikra, ndiyo sababu CHADEMA tunawambia maovu yao ili watambue hisia za wananchi lakini hawataki kuzibua masikio na badala kupongeza wao wanakasirika.Siku zote ukweli unatabia ya kuudhi masikio” alisema Shibuda

Mbunge wa Jimbo la Mawa Magharibi alibainisha kuwa Watanzania masikini wanateswa na viongozi waliopo madarakani kutokana na sera yao ya kutesa kwa zamu, huku uovu ukifanywa funika kombe mwana haramu apite wao wakidai wanajivua gamba.

Alisema viongozi wa CCM na serikali yake ni wavivu na wana hila mbay na desturi mbovu na tabia ya ubinafsi na visasi hali ambayo ni hatari kwa mustakabali wa nchi ndiyo maana upizani umekuwa ukisema yaliyo katika ukweli na uwazi na kisasi cha CCM ndiyo kimeifikisha nchi mahali pabaya kuzaa matabaka.

Alidai kuwa kwa miaka 20 sasa CCM imeshindwa kuandaa viongozi bora baada ya Mwalimu Nyererena katu haiezi kusimama kwa vile imekosa mbegu bora ya uongozi wa kuwatumikia wananchi.

“Naomba niseme, CCM na dola ni wavivu wanatabia mbovu na chafu zisizojenga. Sheikh akiwa mwovu usikasirikie Msahafu na usichome Biblia kwa sababu ya padri mwovu. Hivyo CCM haiwei kusisima, watu wazima hovyo,” alisema Shibuda na kuhoji tangu lini kanzu jeupe likafuliwa kwa sabuni ya mkaa?

Kuhuisu vyama vya upinzani alisema CCM ina deni ya kuvipenda kwa sababu vyote vina muenzi Baba wa Taifa na kueleza mzazi hawezi kumkataa mwanaye na masikini anapaswa kupendwa na tajiri.

Alisema CCM inapaswa kutambua kuwa vyama vidogo vya upinzani vina faida ya maslahi ya Taifa sawa na mgongo wa tembo kumfukuza inzi hivyo vinapaswa kupewa ruzuku.

“Nina mavuno ya utajiri wa kumbaua tulikotoka. Je, tutajikwaa na kuangukia wapi, nitatoa urithi gani kusaidia Watanzania. Siasa si kugombana wala hila na visa.Bima ya haki itapatikana penye haki sawa katika nchi,” alisema Shibuda.

Mbunge huyo pia aliwaasa wazee wa jimbo hilo kutambua thamani yao ya kuitwa wazee bila kuona haya kwani baadhi yao wana matende ya kuwaharibia vijana kwa madai kuwa wamelelewa na CCM.