Mzee Yussuf afungua ‘My Collection’

Duka maalumu litakalofanya kazi za kusambaza kazi za Bendi ya Jahazi

Na Mwandishi Wetu

MSANII wa mziki wa Taarabu nchini Mzee Yussuf ameamua kufungua kampuni yake ya usambazaji ijulikanayo kama ‘MY Collection’ kwa ajili ya kusambaza kazi zake.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Meneja Mauzo wa Kampuni hiyo Mussa Msuba amesema wameamua kufungua duka kwa ajili ya kuuza CD NA DVD za bendi ya Jahazi inayongozwa na Mzee Yussuf duka hilo lililopo makutano ya barabara ya likoma na Muhonda.

linalojihusisha na huzwaji wa DVD za taarabu kwa jumla na rejareja kwa ajili ya kuwaweka karibu wapenzi wake ili waweze kupata burudani kupitia nyimbo zao kwa kuwaburudisha wakiwa majumbani.

Msuba amesema kuwa Mzee yusufu yupo mbioni kutoa albamu yake ya mduara itakayokuwa hivi karibuni ambayo ni yake binafsi mbali na hilo bendi hiyo itatoa video yake ya Live za albamu zake zote za Two in One, Kazi ya Mungu, Nakula ka Naksh Naksh, tupendane, Daktari wa Mapenzi. Ambazo zitakuwa madukani kwa ajili ya kuwapa wapenzi wao burudani wakiwa majumbani mwao.

Naye Mzee Yussuf aliongeza kwa kusema ameanzisha Kampuni yake binafsi baada ya kuona kwamba kazi zake nyingi zimekuwa zikichakachuliwa kutokana na kuwepo kwa wizi wa kazi za Sanaa.

Kampuni yake imekuwa ikisambaza kazi zake kwa ajili ya kuogopa kuibiwa kutokana na wimbi wa kazi za wasanii nchini.

Duka lililopo mtaa wa Muhonda na Likoma kwa ajili ya CD za Jahazi pekee mbali na duka hilo mzee Yusufu anamiliki Duka lingine la Nguo lililopo Magomeni Mapipa kwa ajili ya kujiongezea kipato chake mbali na bendi yake. Bendi ya Jahazi mpaka sasa imekwisha toa albam nane ambazo zipo madukani zinauzwa kwa ajili ya watu wotekupata burudani wakiwa majumbani mwao.

Kwa sasa bendi hiyo ipo mbioni kuachia albamu yake ya tisa ambayo aijapewa jina inatarajiwa kuzinduliwa mwezo October kwa ajili ya kutoa burudani kwa wapenzi wao na kuwataka mashabiki wao kuja kuangalia na kusikiliza nyimbo mpya popote pale wanapotoa burudani zao katika kumbi mbalimbali za jijini Dar es Salaam.