Amsha amsha ya Tamasha la Fiesta ndani ya Tanga

Mtangazaji wa Clouds Fm Adam Mchomvu akionyesha t-shirt ambazo zimetoka kwa ajili ya kusherekea tamasha hilo la Fiesta 2012.
Mwanadada Loveness Love akisababisha ndani ya .
Mkuu wa Vipindi wa Clouds Fm Sebastian Maganga akiendeleza harakati za kukamata matukio ndani ya kitaa cha Chumbageni, pale Clouds Fm ilipotembelea vijana hao wa maskani na kupata mawili mawili matatu kuhusiana na tamasha hilo.
Mazungumzo ya haopa na pale yakiendelea.
…vijana wakimsikiliza Mkuu wa Vipindi wa Clouds Fm Sebastian Maganga, pembeni yake ni Adamu Mchomvu.
Vijana walipata mzuka wa kufunguka na kuonyesha vipaji vyao.
…Mzuka ulipata na kuanza kuchana.
Mmoja ya maproducer wakali wa msanii Moraka akiongea machache mara baada ya kukutwa akiwa amekaa na vijana wenzake ndani ya maskani ya Chumbagenino.
Moja ya staili niliyokutana nayo.
Picha ya Kumbu kumbu kwa vijana wa Chumbagenino.
Mara baada ya Clouds Fm kutoka Kitaa cha Chumbageni maskani ya Chumbagenino Clouds Fm ilihamia kitaa kingine ambapo alijitokeza kijana mmoja na kuomba awe mtangazaji hapa alikuwa alimfanyia mahojiano Mwanadada Loveness Love.
Aha… Sudi Brown (kushoto) akiwa na Mchomvu.

Ukumbusho Muhiumu sana.
Aha…mambo yalinogeshwa na kuwekwa sawa. Unaweza kufuatilia kinachoendelea katika amsha amsha za tamsaha la Fiesta 2012 kupitia Kajunason Blog.