Mwakilishi Mkazi wa UNFPA Bi. Mariam Khan (kushoto) akisalimia umati wa wakazi wa jijini Dar (hawapo pichani) na kutoa ujumbe kwa vijana kuungana na kujiepusha na mangonjwa hatarishi. Kulia Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Tanzania Dk. Elisante Ole Gabriel.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Tanzania Dk. Elisante Ole Gabriel akiwasilisha ujumbe kwa niaba ya Waziri wa Wizara ya Vijana Utamaduni na Michezo ambapo amewataka vijana kujitambua na kuwa na mikakati endelevu na kukaa kama vikundi ili Serikali iweze kuwasaidia kupata misaada na kuwawezesha kuwa na maendeleo endelevu katika siku hii ya maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Vijana Duniani ambayo huadhimishwa kila tarehe 11 Agosti na kutimiza malengo aliyokuwa akiyatafakari baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere juu ya Vijana.
Pichani Juu na Chini Kipute kati ya Mburahati Queens na Evergreen Queens ambapo mchezo huo ulimalizika kwa Evergreen kushinda 2-1.