BAJETI ya elimu itasomwa bungeni siku ya Jumatatu, 13 Agosti. Wakati bajeti ya Elimu inasubiriwa kwa hamu na wadau na hasa wapenda maendeleo ya Elimu, Baadhi ya maeneo nchini bado yanakabiliwa na changamoto kubwa sana hasa hali mbaya ya miundombinu, ukosefu wa vyumba vya madarasa na majengo ya shule ambayo yamesababisha baadhi ya shule kuweka madarasa ya nyasi kama shule ya msingi Selous na Mkapa zilizopo wilayani Namtumbo, Shule ya msingi Silabu iliyoko wilayani Korogwe, Shule ya msingi Misunkumilo ya wilayani Nkasi, na baadhi ya shule wilayani Muleba.
Hali ya elimu imezidi kuwa mbaya kila kukicha, kiasi kwamba hata watu hudiriki kuuliza kama shule hizo zipo nchini, hasa wakiangalia juhudi na kelele nyingi zilizopigwa juu ya mchango mkubwa wa MMEM na MMES kuwa zimefanya kazi kubwa sana kuboresha mazingira ya kujifunzia hasa miundombinu ya shule. Swali Je, shule hizi ziliachwa wapi na mipango hii? Je bajeti ya elimu ya 2012/2013 itatatua baadhi ya changamoto za elimu nchini?na kuondokana na majengo haya yasiyo rafiki kwa mwanafunzi na mwalimu?
Mwana blog, Hebu angalia jinsi ambavyo wanafunzi huko Tanga, Rukwa, Kagera na Ruvuma wanavyojifunza kwenyesehemu zinazokatisha tamaa: Watatoka?