Kinapa wakamata majangili wa mazao ya misitu

Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Robert Boaz

Na Mwndishi wa dev.kisakuzi.com-Moshi

HIFADHI ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) kwa kiushirikiana na polisi mkoani Kilimanjaro wameendeleza operesheni ya kukamata majangili wa mazao ya misitu na wanyama katika hifadhi hiyo lengo likiwa ni kuongeza nguvu ya kudhibiti tatizo hilo na kutoa uelewa wa sheria za misitu na mazingira kwa wananchi.

Kufuatia operesheni hiyo watu wawili wakazi wa mkoani Arusha wamekamatwa katika kijiji cha Lerang’wa mpakani mwa Wilaya ya Longido na Siha mkoani Kilimanjaro kwa tuhuma za kuhusika na vitendo vya kijangili katika eneo la West Kilimanjaro wilayani Siha.

Akitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro Robert Boaz alisema watu hao walikamatwa Agosti Tisa majira ya saa moja na nusu asubuhi baada ya kupata taarifa kuwa kuna watu wamejificha katika kijiji cha jirani.

Kamanda Boaz aliwataja watu hao kuwa ni Mkonde Mhozya (50) na Ezekiel Songoyo ambapo baada ya kufanyiwa upekuzi walikutwa na bunduki moja aina ya Rifle yenye namba za usajili 3754285 na risasi zake 10.

Kwa mujibu wa Kamanda, Boaz Ezekiel songoyo baada ya kufanya uchunguzi walibaini kuwa anakosa lingine la unyang’anyi kwa kutumia nguvu na kwamba kesi iko mahakamani. Alisema uchunguzi unaendelea ili kuweza kubaini uhalali wa silaha waliokamatwa nayo watuhumiwa na kwamba baada ya uchunguzi kukamilika watafikishwa mahakamani.

Akizungumza mhifadhi mkuu wa KINAPA Erastus Lufungulo alikiri kuendelea kuwepo kwa ujangili katika maeneo ya hifadhi na kusema kuwa wanaendeleza operesheni kwa kushirikiana na polisi ili kuhakikisha tatizo hilo linakwisha.

Alisema katika kipindi cha Julay 2011 hadi Jun 2012 hifadhi hiyo imekamata majangili 420, mbao 5,018, Chainsaw nane pamoja na bunduki tatu na kwamba ujangili ambao unaendelea katika hifadhi ni wa mazao ya misitu pamoja na wanyama.